Na:Jonhson Soah
Kampuni binafsi za ulinzi mkoani
singida zimeshauriwa kuimarisha ushirikiano na jeshi la polisi ili kuleta
ufanisi.
Hayo yamesemwa leo na kamanda wa
polisi mkoa wa Singida, ACP Geoffrey Kamwela wakati wa kikao na kampuni binafsi
za ulinzi ofisini kwake, kwa lengo la kubadilishana taarifa juu ya usalama
mkoani hapa.
Kamanda kamwela ameyataja mambo
waliyokubaliana kuwa ni utaratibu wa kuendesha mafunzo ya darasani pamoja na
ukakamavu kwa walinzi binafsi yatatolewa na jeshi la polisi.
Aidha Bw. Kamwela amezitaka kampuni
binafsi kuajiri watu kulingana na uadilifu, na umri unaostahili na kuzishauri
kampuni hizo zipitie jeshi la polisi ili kuhakikishiwa taarifa sahihi za
waajiriwa.
Mkoa wa Sngida una kampuni za ulizni
binafsi zipatazo 18 zilizosajiliwa kisheia.
No comments:
Post a Comment