Na:Edilitruda Chami
Wakazi wa mkoa wa Singida
wameaswa kutotegemea ajira kutoka mashirika binafsi na serikalini badala yake kujiunga na kuanzisha vikundi mbalimbali vya
kijasiriamali ili kujikomboa kiuchumi.
Wito huo umetolewa
na mwenyekiti wa mradi wa mafunzo woman society
mkoani singida bi. Amina Abubakari
wakati akizungumza na standard radio juu ya umuhimu wa kuunda makundi ya
kijasiriamali kwa wanawake katika kujiendeleza kibiashara.
Bi. Amina
amesema lengo la mradi huo ni
kuhakikisha maambukizi ya virusi vya
ukimwi hayaenei kwa kuwawezesha
wanawake kuwajibikaji na shughuli za kiuchumi, kuzuia ongezeko la mimba za utotoni, pamoja na kuwaweka walemavu na watoto wanaoishi katika
mazingira magumu katika hali nzuri ya
maisha kwa kuwajengea uwezo wa kujiajiri wenyewe.
Amesema kila mwananchi atambue umoja ni nguvu na
utengano ni udhaifu kwa kuwashirikisha wananchi wengine katika miradi
mbalimbali ya kimaendeleo, bila kubaguana kwa misingi ya dini, siasa au kabila. Mradi wa mafunzo woman society umeanziasha vikundi vya wajasiriamali wadogo wadogo
15 wanaoshughulika na kilimo, ufugaji na usindikaji wa vyakula, na wameweza
kutoa mafunzo kwa vijana 273.
No comments:
Post a Comment