Na:Mwandishi wetu
Madiwani watano wa
Chama Cha Mapinduzi wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma, wamesema hawatoshiriki
uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, kutokana na
ukiukwaji wa sheria uliofanyika.
Madiwani hao
wametoa kauli hiyo kufuatia uchaguzi wa jina la atakaekuwa mgombea wa kiti
hicho uliofanyika juzi wilayani humo kupitia chama hicho kudaiwa kufanyika
kinyume na utaratibu.
Madiwani hao wamesema
katika uchaguzi wa nafasi hiyo kupitia CCM zilitangazwa nafasi nne pamoja na
kutakiwa kuwa na majina matatu ya wagombea lakini yalitangazwa majina mawili
pamoja na nafasi 2 kitu ambacho ni kinyume na kanuni za chama hicho
Mmoja wa madiwani
hao Bw Alois Edward diwani wa kata ya Biharu amesema baada ya tukio hilo baadhi
ya madiwani walihoji na hawakupata majibu kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi huo
zaidi ya kutishiwa kupokonywa nafasi zao pamoja na kadi za uanachama ambapo
wamesusia uchaguzi huo
.Standard Radio imemtafuta katibu wa chama hicho mkoa wa kigoma Bw Mohammed Nyawenga msimamizi wa uchaguzi huo, ili kuzungumzia tukio hilo na kudai kuwa hayupo tayari kuzungumza lolote na hata alipotafutwa kwa njia ya simu haikupokelewa.
No comments:
Post a Comment