Na:Mussa Mbeho
Wakazi wa mkoa wa singida
wameshauriwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pindi wanapobaini kuwa kuna
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kuwasaidia.
Hayo yamesemwa na Afisa ustawi wa
jamii wa mkoa wa singida Bi. Zuhura Karya
wakati akikabidhi watoto
waliogundulika wakiishi katika mazingira magumu kwa uongozi wa shule ya
msingi St.Vicent iliyopo Itigi wilayani
Manyoni.
Bi. Karya amesema kuwa wananchi
washirikiane na viongozi wa serikali ili kufichua watoto ambao wanaishi katika
mazingira hatarishi ili kuwawezesha watoto kupata haki zao za msingi na si
kuwaacha waendeleee kuteseka.
Aidha amesema kuwa wataendelea kuwasaidia watoto ambao wanaoteseka kwa
kuwalea na kuwasomesha ili kuondokana na tatizo la ongezeko la watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi.
Bi. Karya amewataja watoto waliopatikana
katika mazingira hatarishi kuwa ni Juma Masunga mwenye umri wa miaka 13,
Swalehe Masunga mwenye umri wa miaka 11, Rajabu Masunga mwenye umri wa miaka 8,
na Tabu Masunga mwenye umri wa miaka 6 ambao walikuwa wakiishi na baba yao
aliyekuwa akijulikana kama mganga wa jadi kumbe ana matatizo ya akili.
No comments:
Post a Comment