Na;Iran radio
Tanzania imetangaza kuwa itauomba Umoja wa Mataifa ukipe
mamlaka makubwa zaidi kikosi cha kimataifa cha kulinda amani huko Darfur
(UNAMID) baada ya mauaji ya askari wa wanauhudumu katika kikosi hicho.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali
Kapambala Mgawe amesema kuwa Tanzania inafanya mazungumzo na Umoja wa Mataifa
kuhusu uwezekano wa kikosi cha UNAMID, kupewa mamlaka makubwa zaidi ya kujilinda
dhidi ya makundi yenye silaha huko Darfur, magharibi mwa Sudan.
Wakati huo huo, kamanda wa kikosi cha UNAMID Mohammed Bin
Shampas amesema watu waliofanya shambulizi la Jumamosi iliyopita dhidi ya
askari wa kikosi hicho huko Darfur walikuwa wamejizatiti kwa silaha na ametoa
wito wa kuangaliwa upya uwezo na zana za kikosi hicho.
Askari saba wa Tanzania katika kikosi cha UNAMID waliuawa
Jumamosi iliyopita na wengine 17 kujeruhiwa katika shambulizi la kushtukiza
lililofanywa na watu waliokuwa na silaha dhidi ya kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment