Na;Prisca Rojin
Afisa mhifadhi wa wanyamapori
halmashauri ya wilaya ya Singida Bw. Augustino Lorry, amewataka wananchi kutoa taarifa pale
inapogundulika mtu ameuza nyara za serikali kwa maslahi yake binafsi, ili achukuliwe hatua za kisheria.
Kauli hiyo inafuatia mtu mmoja
anayefahamika kwa jina la Hassan Jumannne mkazi wa mtaa wa Mamtanda Mandewa, anayetuhumiwa
na wakazi wenzake kuhamisha maji kutoka
kwenye bwawa linalotumiwa na wakazi wa eneo hilo na kuuza vyura.
Afisa mhifadhi wa wanyamapori Bw. Lorry,
amesema kuwa mtu huyo amevunja sheria ya
uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ya kuuza nyara za serikali bila
kibali.
Aidha Bw Lorry ametoa tahadhali kwa
jamii nzima kulinda na kutunza wanyama pia kutouza nyara za serikali bila
kibali kutoka kwa maafisa wa wanyamapori.
No comments:
Post a Comment