wananchi
wameaswa kutokubali kuburuzwa na mawazo yanayotolewa na vyama vya siasa, katika
mchakato wa kupata katiba mpya, bali kuzingatia mahitaji ya umma kwa maendeleo
ya taifa.
wito huo
umetolewa leo na baadhi ya viongozi wa vyama vya ccm na chadema wakati
wakizungumza na standard radio, kuhusiana na mchakato wa kupata katiba mpya.
katibu mwenezi
wa ccm mkoa wa singida mwl. musa sima, amesema kuwa kwa sasa hali ilivyo vyama
vya siasa, vinazingatia propaganda za kisiasa ambazo kimsingi zinaegemea kwenye
mahitaji ya chama, kuliko kuegemea katika mahitaji ya jamii, jambo ambalo ni
hatari katika mustakabali wa maendeleo katika taifa hili.
kwa upande wake
katibu mwenezi wa chadema mkoa wa singida mwl. mutta anselim, amesema kuwa
nafasi ya chama cha siasa katika mchakato wa katiba mpya, ni kutoa elimu kwa
wananchi, hivyo wananchi wanatakiwa kupima elimu hiyo, kama inatija kwao ama
la.
aidha wametoa
wito kwa wananchi kusubiri hatua ya mwisho ya kupiga kura ya maoni, katika
rasimu itakayopitishwa na bunge maalum la katiba, kama itakuwa na mambo
wanayoyahitaji ama vinginevyo, ili
kupata katiba inayokidhi mahitaji ya wananchi.
No comments:
Post a Comment