madereva wa malori kutoka nchini wamepata usumbufu
kuingia rwanda kabla ya kuanza kutumika kwa ushuru mpya, wa barabara ambao umeanza
kutumika tena leo, kwa upande wa rwanda ukilenga magari kutoka tanzania tu.
rwanda iliongeza ushuru kwa zaidi asilimia 229,
dhidi ya magari ya mizigo ya tanzania tu kutoka viwango vya zamani vya dola za
marekani 152, hadi dola 500 kwa madai ya kutaka usawa na tanzania.
ushuru huo ambao ulianza kutumika rasmi septemba
mosi mwaka huu, kisha kusitishwa kwa muda, ulitarajiwa kurejeshwa tena leo
kulingana na tangazo la rwanda mpakani rusumo.
mkuu wa wilaya ya ngara, bw. constantine kanyasu,
amethibitisha serikali ya rwanda kuongeza ushuru wa barabara kutoka dola 152,
hadi dola 500 na kwamba baada ya mazungumzo na serikali ya tanzania, walikubali kurejesha kiwango cha zamani,
lakini kwa muda tu.
No comments:
Post a Comment