Na.Mwanishi wetu
Jumla ya wakulima elfu
10 na mia 5 kutoka mikoa 15 hapa nchini wanatarajiwa kunufaika na mradi wa
uwezeshaji wa familia kupitia maendeleo ya kilimo uliofadhiliwa na Bangladesh
kupitia taasisi ya BRAC
Akiongea na waandishi
wa habari mratibu wa mradi huo kanda ya Ziwa Bw George Zabron amesema mradi huo
umeanza mwezi wa April mwaka huu ambapo kila mkulima atapatiwa mtaji kwa mwaka
wa kwanza wa EURO 84
Amesema mradi huo
umelenga kuleta uzalishaji kwa mkulima ambapo watajikita na ufugaji wa kuku wa
kienyeji na mkulima anayelima mahindi kuanzia nusu ekari
Bw Zabron ameongeza
kuwa kila mkulima atakuwa anapewa pembejeo kwa lengo la kuthibiti matumizi
yasiyokuwa sahihi ya mradi huo
No comments:
Post a Comment