Na. Anna Chiganga
Wanafunzi shule za
sekondari mkoani Singida wametakiwa kupenda masomo ya sayansi ili kwenda
sambamba na mabadiriko ya Sayansi na teknolojia
Mwalimu wa sayansi
katika shule ya secondary Mitunduruni Bi.Costantini Bejimula amesema wanafunzi wanaogopa kusoma masomo hayo
kutokana na shule nyingi kutokuwa na maabara na vifaa vya maabara hali inayosababisha wanafunzi kuona masomo hayo kuwa magumu
Aidha amesema wazazi
wanachangia watoto wao kutopenda masomo hayo kwa kueleza kuwa ni magumu jambo
ambalo si la kweli
Hatahivyo ameiomba
serikali kujenga maabara na kuwakea vifaa vya maabara hatua itakayosaidia wanafunzi
kupenda masomo ya sayansi
No comments:
Post a Comment