jumla ya wanafunzi laki nane na sitini na nane elfu
na thelathini wa darasa la saba nchini, wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu
elimu yao ya msingi kesho.
naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, philipo
mulugo, amesema kuwa, mtihani huo utakaojumlisha masomo matano, utafanyika kwa
siku mbili kuanzia kesho hadi kesho kutwa alhamisi.
kati ya idadi hiyo ya wanafunzi waliosajiliwa
kufanya mtihani huo, wavulana ni laki nne na elfu kumi na mbili na mia moja na
tano, sawa na asilimia 47, na wasichana laki nne na elfu hamsini na tano na mia
tisa ishirini na tano, sawa na asilimia 52.52. jumla ya masomo matano yanatarajiwa
kutahiniwa na wanafunzi hao ambayo ni pamoja na kiswahili, kiingereza, sayansi,
hisabati na maarifa ya jamii.
aidha, waziri mulugo pia amewataka wasimamizi
kusimamia kwa umakini na uadilifu, pamoja na kuwaasa wanafunzi wote
kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu wa mtihani, kwani
watakaobainika kufanya hivyo watafutiwa matokeo yao yote ya mtihani.
No comments:
Post a Comment