Friday, November 15, 2013

WATANZANIA ELFU30 HUPOTEZA MAISHA KWA KUTOZINGATIA USAFI


Na.Iman Musigwa
Jumla ya watanzania elfu 30 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na uchafu wa mazingira

 
Katibu wa kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kutoka wizara ya afya na usitawi wa jamii Bw Anyitike Mwakitama amesema hali hiyo inatokana na usafi wa mazingira kuwa ya kiwango cha chini

Amesema tafiti zinaonyesha asilimia 12 tu ya kaya nchini ndio hutumia choo bora, huku asilimia 88 hazina vyoo ama vile vinavyotumika si vyoo bora

 
Katika suala la kunawa mikono utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa asilimia 97 ya kaya hazina sehemu za kunawia mikono katika vyoo vyao hali inayo onyesha kuwa asilimia tatu tu ndio hunawa mikono baada ya kutoka chooni

 
Aidha ametoa wito kwa jamii kubadirika ili kuhakikisha usafi wa mazingira na wa mtu binafsi unadumishwa kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba


No comments: