Tuesday, November 5, 2013

AFUNGWA MIAKA 30 KWA UNYAN'GANYI WA KUTUMIA SILAHA


  Na.Neema Mwampamba
Mahakama ya wilaya ya Singida imemuhukumu Daud Melembeka mkazi wa kijiji cha Mkenene wilaya ya Ikungi kifungo cha miaka 30 gerezani 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya nondo

Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Singida,Flora Ndale  mwendesha mashitaka wa polisi Godwel Lawrance aliiambia mahakama kuwa  tukio hilo lilitokea November 14 mwaka jana kwa kumunyang’anya piki piki Bw Emmanuel Mussa yenye namba T.914 CCS aina ya fekon

Amesema kabla na baada ya kufanya unyang'anyi huo Daud alimtisha kumpiga mlalamikaji Emmanel kwa nondo ili kutekeleza lengo lake

Siku ya tukio Daudi alikodisha pikipiki hiyo na wakati wanaendelea na safari ghafla alimwamuru Emmanuel asimame ndipo akatumia fursa ya kupora pikipiki



Akitoa hukumu hiyo hakimu Ndale amesema mahakma imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa

No comments: