Tuesday, November 5, 2013

TRA SINGIDA YAZINDUA SIKU YA MLIPA KODI



 Na.Mwandishi Wetu
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Singida, imezindua rasmi maadhimisho ya saba ya siku ya mlipa kodi Tanzania,kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo ya kutoa misaada kwa makundi yenye mahitaji maalumu.

Kaimu meneja wa TRA mkoa wa Singida Alistides Paulo, amesema hayo wakati akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya saba ya siku ya mlipa kodi Tanzania kwa mkoa wa Singida.

Katika taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na afisa elimu na huduma kwa mlipa kodi Bw Zakaria Gwagilo,imetaja baadhi ya shughuli zitakazofanyika katika maadhimisho hayo,kuwa ni pamoja na kutoa misaada kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.

Kwa mujibu wa kaimu meneja Paulo,mkoa wa Singida,unatarajia kuongeza makusanyo kutoka shilingi bilioni 4.19 kwa mwaka 2013/2014 zinatajiwa kukusanywa hadi shilingi bilioni  8.3 ifikapo mwaka 2017/2018.

No comments: