Monday, November 4, 2013

MISHAHARA YA WABUNGE WAINGIZA MGOGORO CHADEMA



ZITTO NA LEMA WARALUANA MITANDAONI, WAKAIDI USHAURI WA MNYIKA
....LEMA AKIRI CHADEMA KUUNGA MKONO MSHAHARA KUPANDA
....ZITTO  AENDA NJE KUSAKA UMARUFU AKIPINGA MISHAHARA KWA KUDAI NI CCM WANAODAI NYONGEZA
 
Siku chache baada ya vyombo vya habari kumruka na habari inayodai kuwa Wabunge wa CCM wanadai nyongeza ya Mishahara, Wabunge wawili wa CHADEMA wanaendeleza malumbano kiasi cha kukaidi ushauri wa viongozi wenzao wa chama huku kila mmoja akimlaani mwenzake kwa undumila kuwili.
 
hayo yameibuka jana katika mitandao ya kijamii ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anakwaruzana na Mbunge wa Arusha Gobless Lema kutokana na kile wanachotaja kuwa ZITTO anatabia ya kusaka umaarufu katika hoja zinazoibuka bungeni na kukiuka misimamo ya chama chake

ANGALIA MDAHALO HUU HAPA CHINI

Nov 3 at 8:08 PM
Nimetoka kwenye vikao na Serikali muda huu na kupokea Sms za kwamba kuna suala hili ambapo kauli yangu inahitajika.

Katika hatua hii ya awali nieleze tu kuwa shutuma na tuhuma hizo za Lema kwa Zitto kutolewa kupitia mitandao ya kijamii ni kinyume na kanuni za chama ambazo zimeweka bayana mipaka kwamba viongozi kuhojiana au kukosoana ni kupitia vikao halali vya chama.

Nimewapigia simu wahusika lakini simu zao wote wawili zinaita bila kupokewa. Iwapo yeyote kati yao atasoma ujumbe huu, kabla ya kuendelea kujibishana na kutuhumiana afanye rejea ya katiba.

Kwa wanachama na wapenzi, suala hili litamalizwa katika vikao vyetu vya ndani kama ilivyokuwa kwa masuala mengine ya nyuma. Kuna masuala makubwa muhimu kwa taifa wiki hii ambayo hatupaswi kuachia muda wetu ukatumika kwenye malumbano ambayo yanaweza kuepukwa. Iwapo kuna mwenye malalamiko juu ya yeyote yanayohusiana na mambo ya Bungeni awasilishe rasmi kwa Katibu wa Wabunge wa CHADEMA hatua ziweze kuchukuliwa. Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki viheshimiwe.

JJ
Simu: 0784222222

From: Ansbert Ngurumo <ansbertn@yahoo.com>
Sender: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Date: Sun, 3 Nov 2013 19:19:11 +0300
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com<mabadilikotanzania@googlegroups.com>
ReplyTo: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: Re: [Mabadiliko] Lema Vs Zitto

Sijaelewa aliyenzisha mjadala huu (Lema) alilenga kupata nini. Naendelea kutafakari!
Ansbert Ngurumo
Existential Philosopher, Musician, Journalist & Media Manager
Vox Media Centre & Free Media
Tanzania

On 3 Nov 2013, at 5:59 alasiri, Zitto <zittokabwe@gmail.com> wrote:
Ni mambo ya kuzusha tu yasiyo na maana yeyote. Hayana ushahidi na yamejaa porojo tu. 
Sichukui posho ya vikao popote pale

Sent from my iPhone

On Nov 3, 2013, at 5:54 PM, Nyoni Magoha <john.magoha@gmail.com> wrote:
Nilitoa angalizo...tuvute subira, mbivu na mbovu zitajulikana :))

On Nov 3, 2013, at 9:28 AM, Humphrey Simba <simbahd@gmail.com> wrote:
Nimeitoa jamii forum. .
Mwenye macho na asome wengine mnaweza kuufuata mjadala kule
J Lema 14:15 Today
Kama nilivyosema jana kuwa leo kabla ya saa nane
mchana nitaweka wazi unafiki wa Zitto katika suala la
posho , suala ambalo halihitaji vikao vya Chama kulijadili
isipokuwa vyombo vya habari na hususani mitandao ya
kijamii kama yeye anavyofanya na kujaribu kupotosha
ukweli na kutafuta sifa ambazo kimsingi hana.
CHADEMA wakati inaamua kulijadili suala hili la posho ,
msingi wake mkuu ulikuwa kama ifuatavyo :
1) CHADEMA iliona na kutambua ubadhirifu unaofanyika
kupitia kivuli cha posho katika Taasisi za Umma na
Serikali na sio Bunge pekee , hivyo CHADEMA
ikapendekeza mishahara ipandishwe na posho zisizo za
lazima ziondolewe ili kuondoa mwanya wa ubadhirifu wa
fedha za Umma .Huu ndio uliokuwa msimamo wetu .
Kulikuwa na msingi mkuu ambao ungekuwa na faida
kubwa kwa Nchi na Watu wake lakini kabla msimamo huu
haujawekwa hadharani na kutafsiriwa na Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni , Zitto Kabwe tayari alishatoka katika
vyombo vya habari ni kujipambanua kuwa yeye hataki
posho na wala hatachukua posho , na hapa vyombo vya
habari vilichukua jambo hili kama hoja yake binafsi na
huku mantiki ya hoja kamili ikipotea . ( Mantiki ilikuwa ni
kuondoa posho zisizo za msingi kwa Watumishi wote wa
Umma na kuboresha masilahi yao kwa maana ya
mishahara )
Lengo kubwa la Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa
na CHADEMA ni kupigania masilahi bora ya Watumishi wa
Umma na Sekta binafsi katika Nchi hii . Msingi wa
CHADEMA ulikuwa na maana pevu kwani tulijua kama
mishahara ikiongezwa itampa fursa Mtumishi kuwa na
Maisha bora leo na hata baadaye kwa mafao bora baada
ya utumishi wake kazini . Lakini ingekuwa rahisi pia kwa
Mtumishi kuwa na uwezo mkubwa wa kutafuta mikopo
kwa ajili ya maendeleo kwani Mabenki yanatoa mikopo
kupitia mishahara ya Watumishi . Ikumbukwe kwamba ,
mtumishi mwenye mshahara mzuri anakuwa na fursa ya
kupata mkopo mkubwa ambao utatatua matatizo yake
mengi . Kwa hiyo msingi wa kutaka posho zisizo na
msingi ziondolewe ilikuwa ni mkakati wa CHADEMA
kuboresha masilahi ya Umma kupitia mishahara .
Niliposema Mh Zitto ni mnafiki kuhusu suala hili , nilikuwa
na maana ifuatavyo :
Kwamba , sio kweli kuwa kukataa posho ni uzalendo na
hata ingekuwa ni uzalendo Zitto sio mzalendo katika
suala hili la fedha na maisha yake . Aliposema
hatachukua posho Wananchi wengi walimuona ni shujaa ,
ushujaa ambao hana katika jambo hili . Nasema hivi kwa
sababu , Wakati Zitto anakataa posho ya kikao ya shilingi
sabini elfu ( 70,000 /=) kwa siku ambayo ni sawa na
shilingi takribani milioni kumi na mbili kwa vikao vyote
vya Bunge kwa Mwaka , Zitto huyo huyo , anapokea
posho ya kikao kati ya shilingi laki saba hadi milioni moja
kwa kikao kimoja katika vikao vinvyofanywa na
mashirika mbali mbali hususani Mashirika ya hifadhi za
Jamii . Maana yake ni kwamba kama anapokea laki saba
kwa siku na mashirika haya kwa ujumla wake yakafanya
vikao ishirini tu kwa mwaka na mara nyingi Zitto kama
Mwenyekiti wa PAC huwa anapata mwaliko wa
kuhudhuria vikao hivi , basi atakuwa akipata posho ya
kikao takribani ya shilingi milioni kumi na nne mpaka
milioni ishirini kwa vikao visivyozidi ishirini , wakati kule
juu amekataa posho ya shilingi milioni takribani kumi na
mbili kwa vikao vya siku takribani mia moja na themanini
ambayo ni miezi sita .
Ikiwa vikao hivyo vya mashirika anayohudhuria Zitto
kama Mwenyekiti wa PAC ni vya siku mia moja themanini
kama ilivyo kwa vikao vya Bunge basi Zitto atakuwa
anapokea posho kati ya ya shilingi milioni mia moja na
ishirini na sita elfu na laki sita ( 126,600,000) na milioni
mia moja na themanini ( 180,000,000) . Na hapa naomba
kutaja masilahi yangu katika hili kwani Wabunge wa
kawaida ikiwa wakialikwa katika vikao hivyo huwa
wanalipwa shilingi laki tano kwa kikao kwa siku . Mimi
nimewahi kuhudhuria vikao hivyo mara mbili na nikalipwa
hivyo pamoja na chai na chakula cha mchana . Tofauti na
Mwenyekiti wa Kamati ya PAC yeye pamoja na posho
anayochukua ( 700,000 - 1,000,000) hupewa mafuta ya
gari au tiketi ya ndege yamkutoa alipo na kumrudisha na
kukodiwa Hoteli yenye hadhi ya nyota nne mpaka tano
ambayo kwa siku . Hotel hiyo hulipiwa kati ya dola za
Marekani mia moja mpaka dola mia sita kwa siku .
Ø JE MTU HUYU ANAYEPINGA POSHO YA ELFU SABINI
YA KIKAO CHA BUNGE AMBACHO MSINGI WAKE NI
UWAKILISHI WA WANANCHI NA KUKUMBATIA POSHO YA
YA SHILINGI LAKI SABA HADI MILIONI MOJA YA
MASHIRIKA AMBAYO MSINGI WAKE PENGINE NI
KUWAZIBA MIDOMO WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE
KATIKA MASHIRIKA HAYO NDIYO UZALENDO ? HUU NI
UNAFIKI WAKUTAKA SIFA AMBAZO HAZINA MSINGI.
Lakini huyu Zitto anatoka Jimbo lenye Umasikini mkubwa
ambapo naamini kuwa kuna wahitaji wengi kama yatima ,
wajane , wazee , na wasiojiweza kwa namna mbali mbali ,
kama yeye ni mzalendo kwa nini asingetumia malipo yake
hayo halali kuwasaidia hao ndugu na Jamaa na Wapiga
kura wake ?
Ø NI NA WASI WASI NA UZALENDO ANAOUHUBIRI ZITTO ,
NA AMEPOTEZA MWELEKEO WA HOJA YA MSINGI YA
KAMBI RASMI YA UPINZANI INAYOONGOZWA NA
CHADEMA JUU YA FIKRA SAHIHI YA KUBADILISHA
MFUMO WA KIBADHIRIFU ULIOJIFICHA KWENYE POSHO
ZISIZO ZA MSINGI NA KUBORESHA MASILAHI YA
WATUMISHI WA UMMA KUPITIA MISHAHARA YAO.
MSIMAO WANGU
Kwanza najua na ninamini kuwa “ UMASIKINI SIO
UZALENDO “ sipendi umasikini , nachukia umasikini
lakini pia sipendi kuona mafanikio yangu yanabaki
kwangu tu huku wengine wakiteseka , lakini siwezi pia
kukumbatia umasikini kwa lengo lakuthibitisha uzalendo
wangu.
Najua watu wa Jimbo langu wanataka maji , umeme na
huduma bora za Afya na mambo mengi yenye sura hii
lakini sitang’oa bomba la maji nyumbani kwangu kwa
sababu jirani yangu hana maji ila nimtasaidia kwa kadri
nitakavyoweza na yeye aepukane na adha hiyo ya
ukosefu wa maji .
Najua shule za Kata hazina ufaulu mzuri na mazingira
yake ni magumu , lakini sitampleka mtoto wangu kwenye
shule zisizo na waalimu ili kuonyesha uzalendo bali
nitapigania ubora wa shule hizo kuongezeka ili Wananchi
wote wapate Elimu bora .
Zitto Julai 2012 stahili za Mbunge ziliongezwa kwa
takribani shilingi milioni tatu ambazo ni sawa na milioni
thelasini na sita kwa mwaka , je kwani Zitto hakugoma
kupokea pesa hizo ili kuonyesha uzalendo wake ?
Zitto kuna wakati uliumwa ukapelekwa India kutibiwa ,
sasa kwani hukuwa mzalendo na kufanya mgomo ili
utibiwe hapa Nchini ili kuonyesha Uzalendo wako ? na
kuokoa pesa ya serikali kama ambavyo unaionea huruma
kwenye posho ?
Zitto ningekuelewa , kama maisha unayoishi yangeendana
na kauli zako za Kikomunisti lakini maisha yako na
matendo yako na mienendo yako yanashindwa kutafsiri
kauli zako .
MWISHO – MIMI SIAMINI KAMA MSINGI WA UZALENDO NI
UMASIKINI . LAITI INGEKUWA HIVYO MAKUSUDI YA
KUANZISHA MFUMO WA VYAMA VINGI ILI KUWAKOMBOA
WATANZANI NA LINDI LA UMASIKINI ULIOSABABISHWA
NA CCM YASINGEKUWA NA HAJA , NAJUA ASILIMIA 80
YA WATANZANIA NI MASIKINI SANA , JE WATANZANIA NI
WAZALENDO KWA TAIFA LAO KULIKO WAMAREKANI ?
Namalizia kwa maneno ya Charles Darwin “ If the misery
of the poor be caused not by the laws of nature, but by
our institutions, great is our sin.”
Godbless J Lema
2/11/2013

No comments: