Thursday, May 23, 2013

DW WATOA UDHAMINI KWA STANDARD RADIO FM- USHIRIKIANO WAANZA


Shirika la utangazaji la Ujerumani DW limetoa vifaa vya mawasiiano na utangazaji kwa Standard Radio FM, kama sehemu ya kujenga ushirikiano wa kihabari baina ya Radio za kimataifa Radio za kijamii barani afrika.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 300 vimetolewa mwezi april mwaka huu na standard radio imeanza kuvitumia kuunganisha matangazo ya DW na wasikilizaji wa Standard Radio FM

Sambamba na hayo Standard Radio iliyoko mkoani Singida imetiliana saini ya ushirikiano wa muda mrefu wa kihabari na DW na upo mkakati wa wafanyakazi wa SR fm hususani waandishi wa habari na watangazaji kuanza kupata mafunzo yanayotolewa na kituo cha mafunzo ya kitaaluma cha DW kijulikanacho kama Deutch welle Ackademie

Standard Radio iliyoanza matangazo yake mwezi January mwaka huu imekuwa kwa kasi kufuatia kuwa na mikakati kabambe ya kuhakikisha inakuwa Radio Bora katika eneo la Tanzania na maziwa makuu

No comments: