Tuesday, May 7, 2013

MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AZURU MKOA WA SINGIDA

MAKAMU wa kwanza wa Rais, Serikali ya mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamadi amewataka Watanzania kudumisha upendo baina yao ili kuepuka chuki zinazoanza kujitokeza sasa nchini, kiasi cha kusababisha vurugu na vifo kwa wananchi wasiyo na hatia.
Maalimu Seif amesema hayo mjini Singida, kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani humo iliyoanza May 06 2013 ambapo alipokelewa na viongozi wa serikali na chama cha wananchi CUF mkoani humo.
katika hotuba yake Bw. Seif amesema Watanzania siku zote wamekuwa ni watu wa amani, lakini vurugu zinazoanza kujitokeza sasa siyo za kistaarabu na zinaashiria kuna watu wanaochochea ili kufanikisha malengo waliyokusudia.
Alitumia fursa hiyo kuitaka serikali ya Tanzania kufuatilia kwa makini tukio la ulipuaji bomu katika ibada ya ufunguzi wa kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph mkoani Arusha, ili waliohusika wote wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
PICHA: Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mlozi akimkaribisha jukwaani Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ili kumpa fursa ya kuhutubia umati wa wananchi mjini Singida
 
Aidha alilaani shanbulio hilo la bomu kuiomba Serikali iendelee kulinda usalama wa wananchi wake kwa ajili ya kuenzi misingi imara ya amani, umoja na upendo iliyoasisiwa na waazilishi wa  Taifa la Tanzania.
Makamu wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad alimaliza ziara yake jana na alitarajiwa kuondoka mkoani Singida ili kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

No comments: