Saturday, May 18, 2013

WASOMI KUTOKA KIGOMA WALIA NA WABUNGE WAO



Wabunge wa mkoa wa Kigoma wamehimizwa kujenga umoja na kuwa na mkakati maalumu wa kuutetea mkoa wa Kigoma na kuepuka ushabiki wa kisiasa ambao unatajwa kuiangamiza Tanzania
 
 
 
Raia hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Amos Nyandwi (pichani hapo juu) mchumi kutoka wizara ya kazi na ajira ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma katika kongamano la vijana wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini ambao ni wazawa wa Kigoma
 
Bw. Nyandwi amebainisha kuwa kwa sasa wabunge wote wa majimbo na viti maalumu kutoka mkoa wa kigoma  hawajaonesha umahili wao katika kubuni na kusimamia mipango ya maendeleo kwa njia ya umoja kama wawakilishi wa wanakigoma Bungeni
 
Amesisitiza kuwa licha ya kuwepo na wataalam walioajiliwa serikalini na katika sekta binafsi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisaidia kuchochea wabunge hao kuungana na kuwatumia wataalamu kuibua na kusimamia maendeleo lakini hakuna mwitikio wa wabunge hao
 
Aidha Nyandwi ameonya juu ya wanasiasa kung’ang’ana na vyma vya siasa na kushindwa kusimamia maslahi ya wananchi ambao ndio waliowapigia kura
 
Pamoja na lawama hizo kwa wabunge na wanasiasa, mchumi huyo amewahimiza wasomi walioko katika vyuo kufikiri kurejea mkoani Kigoma na kuunda au kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ii kunufaika na mipango ya serikali ya uwezeshaji jamii kiuchumi.
 
 
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa makampuni ya Buhanzo na Standard Voice limited Bw. James Japhet (pichani hapo juu) amewaonya wasomi kutoka Kigoma kuondoa fikra za kutaka kuajiriwa badala yake wasome kwa umakini na watumie alimu yao kwa ajili ya ujasiriamali
 
Bw. Japhet ameongeza kuwa mkoa wa Kigoma una vyanzo vingi vya uchumi ambavyo havijatumika kuwainua wakazi wa mkkoa wa Kigoma hususani mazao ya ziwa Tanganyika, kilimo, ufugaji na fursa za biashara katika mipaka ya nchi jirani za Burundi, DRC na Zambia.
 
Aidha Bw. Japhet amewataka wabunge wa mkoa wa Kigoma kuungana pamoja kutetea ujenzi wa barabara pamoja na mkoa kuunganishwa na umeme wa gridi ya taifa, na kwamba bila miundombinu ya umeme na barabara za uhakika Kigoma haitapata maendeleo endelevu.
 
 
Zaidi ya wanafunzi 80 kutoka vyuo vya SAUT, Udom, SUA, Mzumbe, St. John, RUAHA na Tumaini wamehudhuria kongamano hilo, ambapo ni mbunge mmoja tu kutoka jimbo la Muhambwe Bw. Felix Mkosamali (pichani aliyekaa katikati juu) aliyejitokeza kushiriki.

No comments: