Wednesday, June 5, 2013

MTOTO MCHANGA ATELEKEZWA NA MAMAE MJINI SINGIDA


Mtoto anaekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita ameokotwa akiwa ametupwa katika kitongoji cha unyakumi kata ya mandewa mkoani Singida

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo afisa mtendaji wa kijiji hichi bi.Hadija Msumari amesema mtoto huyo wa jinsia ya kiume  ameokotwa katika nyumba iliyokuwa ikijengwa  ya bwana Sadiki juma.

Amesema baadhi ya vitu alivyokutwa navyo ni pamoja na begi dogo la nguo,chupa ya uji,na kadi ya kliniki


Akifafanua zaidi amesema kadi ya mtoto inaonesha kwa mara ya mwisho alipelekwa katika kliniki ya uhasibu mjini singida na anaishi kitongoji cha misake na mwenyekiti wa eneo hilo ni bwana Hamisi Mdadi huku jina la mtoto na wazazi likiwa limefutwa

Nyumba alimookotwa mtoto alietelekezwa na mama yake

Aidha mmoja wa mashuhuda ambae amemuokota mtoto huyo bi.Hadija  shabani amesema alikuwa akipita jirani na eneo la tukio majira ya saa mbili asubuhi na kumsikia mtoto akilia kwa muda mrefu ndipo bila kuhisi dalili yoyote ya msaada  ndipo alipoamua kuingia ndani na kumkuta mtoto akiwa peke yake

Jeshi la polisi mkoani singida limemchukua mtoto huyo kufanya uchunguzi ili kumbaini anaehusika na tukio hilo la kinyama
 
Imeandikwa na Edilitruda Chami

3 comments:

Unknown said...

kwanini wa2 wanakuwa na roho ya kinyama kiasi hicho?
Watanzania na wanasingda wenzangu kuweni na huruma bac kwa viumbe wote. Leo hii amem2pa mtoto sembuse ng'ombe na vingne atavionea huruma kweli!

Anonymous said...

hivi huyu mwanamke yy angetupwa akiwa mdogo anazani raha anazozipata angezpata wap tuwe na huruma wanawake jaman na wanaume kuweni makini na hz mambo jaman dhambi ni kwa wote

Anonymous said...

motto mzuriiii na wanaume mnakera bwanaa mkishatia mimba hamtazami nyuma