Wednesday, June 5, 2013

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KWA USTAWI WA JAMII



pichani ni viongozi wa serikali ya wilaya ya Iramba pamoja na Meneja wa Standard Radio fm, Bw. Prosper Kwigize (katikati mwenye Kaunda suti) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tamasha la kuitangaza Radio hiyo wilayani Iramba
Wakazi wa wilaya ya Iramba mkoani Singida, wametakiwa kuitumia Standard Radio katika kufikisha ujumbe kwa jamii na kushiriki kikamilifu katika uandaaji wa vipindi vya kuelimisha umma.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahaya Nawanda, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu tawala wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Naniya, wakati wa utambuilisho wa Standard radio kwa wakazi wa wilaya hiyo uliofanyika katika stendi ya mabasi ya mjini Kiomboi.

Katibu tawala wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Nania (mwenye suti na miwani) akijiandaa kutoa hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iramba Bw. Yahya Nawanda)
Amesema mawasiliano ni kitu muhimu katika jamii kwani hurahisisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na kufikisha ujumbe kwa haraka, lamoja na kuweza kujipatias wateja wengi kutokana na kujitangaza kibiashara.
Awali meneja wa Standard radio Bw. Prosper Kwigize amesema, Standard radio ipo ili kukidhi haja ya wakazi wa mkoa wa Singida kwani ni radio ya kwanza kuanza kutangaza ndani ya mkioa wa Singida tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
 
Bw. Kwigize amesema msimamo wa Standard radio haugemei upande wowote kidini, kisiasa au kijamii, bali ni radio ambayo inatoa huduma zake kwa wananchi wote bila ubaguzi, na kuwataka wakazi wa wilaya ya Iramba kuitumia ipasavyo.

 

No comments: