Tuesday, July 3, 2012

PICHA YA MNARA BAADA YA UJENZI

Hili ndilo eneo la urushaji wa matangazo ya Standard Radio Fm 90.1 Mjini Singida, matangazo yataanza kuruka hewani hivi karibuni, Kwa wakazi wa mkoa wa Singida huu ni ukombozi mkubwa na wa pekee kwani tangu uhuru hakuna radio inayorusha matangazo yake kutoka Mjini Singida.

Hata hivyo sisi SR Fm tunatoa pongezi za dhati kwa kabisa kwa wakazi wa mkoa wa Singida ambao mmeipokea nia yetu kwa shangwe, tunayo hakika kuwa mtashirikiana nasi pia katika kutekeleza malengo yetu

mitambo hii ipo eneo la VETA Singida kiasi cha mita 600 nyuma ya majengo au eneo la VETA, hata hivyo matangazo yatafanyika eneo la GENERY ambako studio zimejengwa


No comments: