Waziri wa mawasiliano ysayansi na teknolojia profesa Makame
Mbalawa, ametoa wito kwa vyombo vya utangazaji kuepuka kutangaza zaidi muziki
na matangazo ya nje ya nchi badala yake vipindi na habari zinazowahusu
watanzania zipewe kipaumbele zaidi
Profesa makame amesema hay oleo jijini Dar es salaam wakat
akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa watangazaji nchini pamoja na mamlaka ya
mawasiliano Tanzania TCRA
Amebainisha kuwa, vyomboo vingi vya habari hasa radio na
televisheni vimekuwa vikitoa nafasi kubwa ya kutangaza muziki na vipindi vingi
kutoka nje ya nchi jambo ambalo linawanyima watanzania kujifunza mambo
yanayowahusu
Aidha ametoa wito kwa watangazaji wote Tanzania kuwapa
kipaumbele watanzania wa vijijini kwa kuandaa vipindi na matangaza ambayo
yatawasaidia kubadilika kimaendeleo kutka walipoo kwa kutumia vyombo vya habari
Hata hivyo profesa Mbalawa ameonya uwepo wa ukiukwaji wa
maadili ya utangazaji na kutoa wito kwa watangazaji wote kutumia fursa ya
matangazo ya mfumo wa digitali kusimamia vema maadili ya taaluma ya utangazaji.
Tanzania imeazimia kuzima mitambo ya mfumo wa analogia na
kuwasha digitali ifikapo desemba 31 mwaka huu kwa mikoa ambayo huduma hiyo
inapatikana.
1 comment:
Nawaunga mkono wadau wote mnaotuhabarisha kupitia blog hii kwani mnatupa habari moto moto. Naunga mkono wito ambao umetolewana Waziri, ni kweli sisi wadau wa habari hasa Watangazaji kuna mahali tunajisahau kuwa sisi ni SAUTI ya WASIO na SAUTI, kumbe basi wadau tuungane pamoja katika kutekeleza wito wa Waziri kwa lengo la kuikomboa nchi yetu.
Post a Comment