Wednesday, September 25, 2013

MSALABA MWEKUNDU MULEBA LATOA MABLANKET 30 KWA RAIA WA KIGENI



Na mwandishi wetu
Shirika la Msalaba Mwekundu wilayani Muleba Mkoani Kagera limetoa msaada wa mablanketi 30 kwa raia wa kigeni waliokuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria waliotokea wilayani humo na kurejeshwa katika mataifa yao
Mkuu wa kitengo cha maafa wa shirika la Msalaba Mwekundu wilayani Muleba Bw Rafael Mbekenga, amesema kuwa mablanketi hayo yana thamani ya Sh laki 9 na kwamba yametolewa wiki iliyopita
Amesema kuwa mablanketi hayo yametolewa kwa raia hao wa kigeni ili yawasaidie kujikinga na baridi wakati wakiwa safarini kurejea katika mataifa yao
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Bw Limbrace Kipuyo, amethibitisha kupokea msaada huo kwa ajili ya raia hao wa kigeni huku akisema kuwa umefika kwa kuchelewa kwa kuwa tayari raia 200 walisharejeshwa makwao


No comments: