Wednesday, October 23, 2013

WAHUKUMIWA MIAKA 30 KWA KUTEKA MAITI





majambazi wakipelekwa magereza baada ya kuteka maiti



Na.Edilitruda chami
Watu wanne wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la unyanganyi wa zaidi ya shilling milioni nane kwa kutumia silaha

Akisoma hukumu hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya mkoani Singida Flora Ndale amesema tukio hilo limetokea desember 8 waka 2012 katika barabara ya singida kwenda Dodoma maeno ya kisaki

Amesema siku ya tukio washtakiwa waliweka mawe barabarani na kuteka gari lililokua likisafirisha maiti ya mwanafuzi wa chuo kikuu cha Sokoine {SUA] kutoka morogoro kuelekea Tarime

Katika tukio hilo vitu mbalimbali kama laptop, simu za mkononi, moderm mbili zote vikiwa na thamani ya shilingi milioni nane laki saba viliibwa

Amewataja waliohukumiwa kuwa ni Hamisi Issa, Halidi Hamisi, Abbubakari Jumanne, Hamisi Alli wote wakazi wa mkoa wa Singida,ambapo siku ya tukio walikuwa na rungu,mawe na mashoka wakitumia kufanya uhalifu huo
Hakimu Ndale amesema kitendo hicho ni amesema adhabu hiyo itakua fundisho kwa watu wengine wanaofanya vitendo kama hivyo.

MSAKO MAALUM KWA WANAOISHI KINYUME NA SHERIA MKOANI SINGIDA





 Na.edson raymond

Mkoa wa singida unatarajia kuanza operation ya ukaguzi wa kubaini watu wanaoishi nchini kinyume na sheria.

Hayo yamebainishwa jana na Afisa uhamiaji mkoa wa Singida Bw. Adam Mnyeke wakati akizungumza katika siku maalum ya polisi iliyofanyika katika ukumbi wa Aquar Manispaa ya Singida,

Bw. Mnyeke amesema kuwa zoezi hilo linatarajia kuanza wiki ijayo, hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ili kupambana na wahamiaji haramu.

Amesema kwa kuanza, zoezi hilo litaanzia manispaa ya singida na baadaye litakwenda katika wilaya nyingine za mkoa wa Singida, na kuongeza kuwa zoezi hilo pia litasaidia kupambana na vitendo vya uhalifu ambavyo mara nyingi vimekuwa vikifanywa na wahamiaji haramu.

Friday, October 18, 2013

BILIONI MIA MBILI NA KUMI NA SABA KUTUMIKA KATIKA UJENZI WA KUFUA UMEME WA UPEPO





  Na.Mwandishi wetu

Jumla ya shilingi bilioni 217 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa upepo
Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini Bw Eliakimu Maswi amesema hayo jana wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu mpango wa matokeo makubwa sasa yaani (Big Result Now)
Mradi huo ambao unatekelezwa kupitia shirika la maendeleo ya taifa NDC, Taneco pamoja na kampuni ya Power pool East africa uko katika hatua za kubadirisha matumizi ya eneo utakapojengwa mradi huo
 
Amesema kuwa baada ya zoezi hilo kukamilika utekelezaji wa mradi huo utaanza mara moja kutokana na kile alichokieleza kuwa tayari mkopo umepatikana kutoka benk ya Exim ya China

WANANCHI WATAKIWA KUWAPA FURSA VIJANA YA MAWAZO KATIKA KAZI




Na.Edilitruda chami
Wananchi mkoani Singida wametakiwa kuwaheshimu vijana wanaofanya kazi katika sekta mbalimbali bila kujali umri wao ili wanufaike na matunda ya kazi hizo
Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Singida Bw Amosi Makala baada ya kugundua  kuwa baadhi ya wananchi hawafiki  katika ofisi za ustawi wa jamii kupata ushauri nasaha pindi wanapokuwa na tatizo

Bw  Makala amesema baadhi ya watu kama vile wazee  hudharau ushauri wanaopewa na wafanyakazi vijana katika ofisi za ustawi wa jamii kwa kuangalia umri na umbo jambo ambalo ni hatari katika utendaji kazi na linalokwamisha maendeleo mkoani Singida

Amesema, ni vyema wananchi kufahamu kuwa endapo hawatafuata ushauri wanaopewa na ustawi wa jamii au kuogopa kufika ofisi hizo wanapokumbana na matatizo mbalimbali kutachangia ongezeko la vitendo vya ukiukaji wa haki za kibiinaadamu