Friday, November 15, 2013

UTUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUWA WAADILIFU

Na.Iman Musigwa
 
Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi Celina Kombani amewataka wahitimu wa chuo cha utumishi wa umma kuonyesha uwezo wa kufanya kazi kwa kujituma na kumudu majukumu yao kwa uadirifu

 
Bi Kombani amesema hayo leo katika mahafari ya 16 ya chuo cha utumishi wa Umma ambayo yamefanyika katika tawi  la singida na kuwajumuisha  wanachuo wa utumishi tawi la Taboraoja pamoja na Singida

 
Aidha amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kutoa huduma bora kwa wananchi

Akizungumzia kuhusu ajira Bi Kombani amesema serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu wanaomaliza katika chuo hicho kulingana na mahitaji ya serikali kwa wakati husika

No comments: