Na.Iman Musigwa
Jumla ya watanzania elfu 30 hupoteza maisha kila mwaka
kutokana na uchafu wa mazingira
Katibu wa kampeni ya kitaifa ya usafi
wa mazingira kutoka wizara ya afya na usitawi wa jamii Bw Anyitike Mwakitama
amesema hali hiyo inatokana na usafi wa mazingira kuwa ya kiwango cha chini
Amesema tafiti zinaonyesha asilimia 12 tu ya kaya nchini
ndio hutumia choo bora, huku asilimia 88 hazina vyoo ama vile vinavyotumika si
vyoo bora
Katika suala la kunawa mikono utafiti wa hivi karibuni
unaonesha kuwa asilimia 97 ya kaya hazina sehemu za kunawia mikono katika vyoo
vyao hali inayo onyesha kuwa asilimia tatu tu ndio hunawa mikono baada ya
kutoka chooni
Aidha ametoa wito kwa jamii kubadirika ili kuhakikisha
usafi wa mazingira na wa mtu binafsi unadumishwa kwa kuwa kinga ni bora kuliko
tiba
No comments:
Post a Comment