Na.Edson Raymond
Kata
ya mtamaa manispaa ya Singida inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vyoo bora
hali inayoweza kusababisha kutokea kwa magonjwa ya miripuko ikiwemo
kipindupindu.
Uchunguzi
uliofanywa na standard radio katani hapo umebaini kuwa kati ya kaya tano hadi
kumi ni kaya moja tu ndiyo yenye choo bora huku kaya nyingine zikiwa zinatumia
vyoo visivyo bora na nyingine kutumia vyoo vya majirani au vya taasisi za elimu
kama vile shule.
Baadhi
ya wakazi walihojiwa na standard radio wamesema kukosekana kwa vyoo bora
kumesababishwa na kukosekana kwa elimu huku wengine wakisema vyoo vingi
vilibomolewa na mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu
No comments:
Post a Comment