Friday, November 15, 2013

HATIMAYE VIWANGO VYA NAULI KWA VYOMBO VYA USAFIRI WA MAJI


Na.Edson Raymond
Mamlaka ya usimamizi wa vyombo vya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA inatarajia kuweka viwango vya nauli kwa vyombo vya usafiri ambavyo hapo awali vilikuwa vinajipangia bei bila kuingiliwa na mamlaka hiyo

 
Afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Singida Bw. Daniel Chilongani amesema hayo katika kipindi cha hoja ya leo kinachorushwa na standard redio

 
Amesema mpango huo utasaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumiaji wa vyombo hivyo

 
Miongoni mwa vyombo vya usafiri ambavyo vitawekewa kiwango maalum cha nauli ni pamoja na Bajaji, Pikipiki maaruf kama Bodaboda pamoja na Taxi ambavyo awali vilikuwa vinajipangia bei zao wenyewe bila SUMATRA kuhusika.

 
Bw. Chilongani amesema kuwa ili kufanikisha jambo hilo kifaa maalum kitafungwa katika chombo hicho ambacho kitakuwa kinahesabu Kilomita na msafiri atatakiwa kulipa nauli kutokana na umbali utakaoonyeshwa na kifaa hicho

 

 

No comments: