Mahakama ya wilaya ya Singida imemuhukumu Daud Melembeka mkazi wa kijiji cha Mkenene wilaya ya Ikungi kifungo cha miaka 30 gerezani 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya nondo
Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Singida,Flora Ndale mwendesha mashitaka wa polisi Godwel Lawrance aliiambia mahakama kuwa tukio hilo lilitokea November 14 mwaka jana kwa kumunyang’anya piki piki Bw Emmanuel Mussa yenye namba T.914 CCS aina ya fekon
Amesema kabla na baada ya kufanya unyang'anyi huo Daud alimtisha kumpiga mlalamikaji Emmanel kwa nondo ili kutekeleza lengo lake
Siku ya tukio Daudi alikodisha pikipiki hiyo na wakati wanaendelea na safari ghafla alimwamuru Emmanuel asimame ndipo akatumia fursa ya kupora pikipiki
Akitoa hukumu hiyo hakimu Ndale amesema mahakma imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka hivyo kumtia hatiani mtuhumiwa
No comments:
Post a Comment