Friday, November 1, 2013

WAFANYAKAZI WAHUSISHWA NA WIZI WA SH.MILIONI 220


 
Na.Mwandishi wetu
Uchunguzi wa awali umeonyesha baadhi ya wafanyakazi walihusika katika tukio la uporaji wa Shilingi milioni 220, mali ya kampuni ya ujenzi ya Dott,

 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, amesema kuwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo inayojenga barabara ya Same-Mkumbara kwa kiwango cha lami, wanadaiwa kuhusika na kuandaa njama za mpango wa uporaji wa fedha za mwajiri wao

Katika tukio hilo lililotokea mapema wiki hii watu wanaodaiwa kuwa  majambazi walivamia gari na kumteka Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo, Shuresh Bab ambaye  alikuwa akisafirisha fedha hizo bila ulinzi baada ya kuzitoa benki



Wakati uchunguzi huo wa awali wa polisi ukibaini hayo, bado  wakazi wa mji wa Moshi wanahoji zilipo  Shilingi milioni 140 kati ya milioni 220 zilizoporwa, licha ya polisi kusema wameokoa Shilingi milioni 80.



 

No comments: