Na.Edson Raymond
Kata ya mtamaa manispaa ya Singida
inatarajiwa kuunganishiwa nishati ya umeme wa grid wa taifa kupitia mradi wa
umeme vijijini REA ili kukabiliana na umasikini wa kipato kwa wananchi wa kata
hiyo.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa CCM Bw. Hassan
Mazala wakati akizungumza na wananchama wa CCM katika kata hiyo ambapo amesema
upembuzi yakinifu juu ya mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi huu.
Amesema kuwa endapo umeme
ukiunganishwa katika kata hiyo kutasaidia wananchi kujishughulisha na shughuli
za kiuchumi ambazo zinategemea nishati hiyo na hatimaye kuondokana na umasikini
wa kipato unaowakabili wakazi wa kata hiyo
Aidha Bw Mazala ametoa wito kwa
wananchi wa kata hiyo kuwa tayari kuonyesha nia ya kuhitaji huduma hiyo kwa
kujiandikisha hali ambayo itaongeza juhudi za mradi huo wa REA kwenda kasi
kutokana na mahitaji ya idadi kubwa ya watu.
No comments:
Post a Comment