Na.Iman Musigwa
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha jana amewaongoza
maofisa wa JWTZ katika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Luteni Rajab Ahmed
Mlima.
Luteni Mlima, aliuawa akiwa na wanagambo wa Kundi la waasi wa M23, katika
Milima ya Gavana, karibu na Goma, chini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani.
Viongozi wengine walioshiriki katika kutoa heshima zao za mwisho kwa
ofisa huyo, ni pamoja na Mnadhimu mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samuel Albert
Ndomba na viongozi mbalimbali wa Serikali
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa heshima hizo, Waziri
Nahodha amesema taifa limepoteza mtu shujaa aliyekuwa akitetea roho za watu.
Amesema Serikali haitarudi nyuma katika masuala ya ulinzi wa amani, na
kwamba itaendelea kutoa msaada wa ulinzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo hadi hapo amani itakapopatikana.
No comments:
Post a Comment