Na.edson raymond
Mkoa wa singida unatarajia kuanza
operation ya ukaguzi wa kubaini watu wanaoishi nchini kinyume na sheria.
Hayo yamebainishwa jana na Afisa
uhamiaji mkoa wa Singida Bw. Adam Mnyeke wakati akizungumza katika siku maalum
ya polisi iliyofanyika katika ukumbi wa Aquar Manispaa ya Singida,
Bw. Mnyeke amesema kuwa zoezi hilo
linatarajia kuanza wiki ijayo, hivyo kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano
kwa taasisi hiyo ili kupambana na wahamiaji haramu.
Amesema kwa kuanza, zoezi hilo
litaanzia manispaa ya singida na baadaye litakwenda katika wilaya nyingine za
mkoa wa Singida, na kuongeza kuwa zoezi hilo pia litasaidia kupambana na
vitendo vya uhalifu ambavyo mara nyingi vimekuwa vikifanywa na wahamiaji
haramu.
No comments:
Post a Comment