Na.Mwandishi wetu
Zaidi ya watu 50 wakiwamo watumishi wa serikali wamekamatwa katika operesheni ya kitaifa ya kusaka wawindaji haramu na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.
Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na kikosi hicho katika mikoa ya Simiyu, Manyara, Mara na ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kesi za washitakiwa hao zimesajiliwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Safina Simufukwe na Hakimu wa Wilaya Mkuu, Hamadi Kasonso.
Ilielezwa kuwa washitakiwa hao kwa nyakati na maeneo tofauti walikamatwa na kikosi hicho wakiwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Washitakiwa hao wanashitakiwa kwa makosa ya kuingia katika hifadhini, kukutwa na nyara za serikali na kuendesha uwindaji haramu kinyume cha sheria
No comments:
Post a Comment