Na.edson raymond
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko
Kone amekanusha taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kuwa mkoa wa Singida
unakabiliwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
kutoa ufafanuzi huo
kutokana na baadhi ya washiriki waliohudhuria katika kikao cha siku maalumu ya
polisi kudai kwamba mkoa wa singida unakabiliwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi
Aidha amesema tangu mwaka 2008 mkoa wa
singida umekuwa ukipambana na changamoto hiyo ya watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi
Amesema mafanikio ni makubwa kwani mkoa
kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Outreach International umefanikiwa
kujenga kituo cha Kids Center kinachotumika kuwapatia huduma muhimu watoto hao.
Dr Kone ametoa wito kwa wakazi wa mkoa
wa singida kuwakamata watoto hao pindi wanapowaona na kuwafikisha katika kituo
hicho, kwani kimejengwa kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kama vile elimu ya
awali, na mahitaji mengine
No comments:
Post a Comment