Thursday, October 24, 2013

UZEMBE KWA BAADHI YA VIONGOZI HUCHANGIA KUZOROTESHA MAENDELEO



Na.Neema julius
 Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi Fatuma Hasan Toufiq amesema chanzo cha kuzorota kwa maendeleo vijijini ni kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya viongozi na kusababisha ushirikiano duni kati ya wananchi na viongozi hao

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa tarafa ya kilimatinde wilayani manyoni Bi Fatuma amesema kuwa ushirikiano duni kati ya viongizi maeneo ya vijijini ni kutokana na ushirikishwaji duni wa shuguli zenye tija kwa jamii na kusababisha miradi ya maendeleo kutofika kwa wakati katika vijiji vya wilaya ya manyoni

Aidha Bi Toufiq ameitaka idara ya ujenzi wilayani hapo kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa wilayani kabla ya mingine kuanza kutekelezwa kutokana na baadhi ya majengo kutokuwa na viwango jambo ambalo linasababishwa na  idara hiyo kwa kuendeleza uzembe na kusahau kutembelea maeneo ya vijijini

Kwa upande mwingine amewataka viongozi wa idara hiyo kujirekebisha ili majengo yaweze kukidhi viwango kulingana na maelekezo ya serikali

No comments: