Na.Neema julius
Mtu mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi kifuani na mwingine kujeruhiwa mikono yote miwili baada ya watu wasiojulikana kuwavamia na kutaka kuwapora mali katika wilaya ya manyoni mkoani Singida
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Igwamadete kata ya iseke tarafa ya Nkonko wilayani manyoni baada ya mtu aliyejulikana kwa jina la Alody Joshua mwenye umri wa miaka 29 kupigwa risasi na majambazi hao
Aidha Daudi Azaliwa amejeruhiwa mikono yote miwili baada ya kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakitoka kwenye mnada wa Mpapa kuelekea nyumbani ndipo majambazi hao walipoanza kuwapiga na kuwanyanganya fedha na kusababisha kifo cha mtu huyo
Jeshi la polisi wilayani manyoni limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa watu watatu wanashilikiwa kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo na kwamba wanatarajiw akufikishwa mahakamani baada ya upelelzi kukamilika
No comments:
Post a Comment