MRAKIBU WA POLISI BW.JAMES KASUSURA
Na.Edson Raymond
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa
minne nchini iliyofanikiwa kupambana na vitendo vya uhalifu kwa kiwango kikubwa
kwa kipindi cha hivi karibuni.
Mrakibu wa Polisi kutoka makao makuu Dar es salaam
kitengo cha maadili James Kasusura amesema hayo wakati akizungumza na washiriki
wa kikao cha siku maalum ya polisi kilichofanyika katika ukumbi wa Aquar
manispaa ya Singida.
Kasusura ameyataja makosa
yaliyopungua kuwa ni makosa dhidi ya ubinadamu ambayo yamepungua kwa asilimia
35, makosa dhidi ya mali yamepungua kwa asilimia 18, makosa dhidi ya maadili
yamepungua kwa sailimia 13, na makosa dhidi ya usalama barabarani yamepungua
kwa asilimia 12.
Amesema kupungua kwa makosa hayo
kumetokana na ushirikiano baina ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani
Singida, hivyo kutoa wito wa kuendelezwa kwa ushirikiano huo na hatimae kukomesha
vitendo hivyo kabisa.
No comments:
Post a Comment