Thursday, May 23, 2013

STANDARD RADIO AUDIENCE- THIS WEEK


Pageviews by Countries

Entry
Pageviews
Tanzania
157
United States
132
Canada
16
Germany
7
France
7
United Kingdom
7
Brazil
6
South Korea
3
Russia
3
India
2

Pageviews by Browsers

Entry
Pageviews
Firefox
123 (26%)
Opera
118 (25%)
Chrome
115 (25%)
Internet Explorer
74 (16%)
Safari
19 (4%)
Mobile Safari
8 (1%)
Dolfin
1 (<1%)
OS;FBSV
1 (<1%)

 

 
 

 

BBC YABISHA HODI STANDARD RADIO FM - MCHAKATO WA USHIRIKIANO WAANZA


Na Boniface Mpagape.

 
Standard Radio FM iliyopo mjini Singida, imeanza mchakato wa kushirikiana na Shirika la utangazaji la Uingereza BBC katika kurusha baadhi ya vipindi na matangazo kutoka shirika hilo.

Hali hiyo imedhihirika baada ya Shirika la BBC Media Action kutuma afisa utafiti wake Bi. Suzy Matamwa ambaye kulingana na maelezo yake mbele ya watumishi wa Standard radio atakuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na kila mwandishi kuhusiana na shughuli za kila siku zinazofanyika katika masuala mbali mbali ya uandaaji wa habari na vipindi mbalimbali.

 


 PIC 1. Bi. Suzy Matama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Standard Radio katika ofisi za SR FM. Kutoka kulia ni Meneja wa SR Bw. Prosper Kwigize, Mkurugenzi wa SR Bw. James Daud na Bi. Suzy Matama kutoka BBC Media Action, wakati akitambulishwa rasmi.


Naye meneja wa Standard radio Bw. Prosper Kwigize amesema kuwa Standard radio inatangaza vipindi mbali mbali vinavyoigusa jamii moja kwa moja katika nyanja mbali mbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo, uchumi, ambavyo hutangazwa na redio hiyo.

Aidha amesema standard radio imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali vya uandishi wa habari hapa nchini.
 
Amesema hivi sasa kuna wanafunzi wanne waliopo katika mafunzo kazini na kwamba wengine waliokuwepo wamemaliza muda wao na kurejea kwao na kwamba zaidi ya wanafunzi watango kutoka chuo kikuu cha mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza wanatarajia kuanza mafunzo kwa vitendo ndani ya Standard radio hivi karibuni

Afisa utafiti huyo kutoka shirika la BBC Media Action, amesema atakuwa akizungumza na wafanyakazi wa standard radio kwa nyakati tofauti kwa muda wa siku tatu, kuhusu masuala ya kawaida kama uandaaji wa vipindi, habari na kurusha matangazo kwa ujumla.

Endapo mpango huo utafanikiwa itakuwa ni fursa nzuri kwa wakazi wa Singida kuweza kusikika katika ngazi ya kimataifa kupitia BBC kwani nao pia watapata fursa ya kuchangia maoni yao kuhusu masuala mbali mbali katika jamii.

Watumishi wa Standard radio pia watanufaika kwa kupatiwa mafunzo pamoja na vitendea kazi ili kuwezesha ufanisi katika kazi za kila siku za kuhabarisha na kuelimisha jamii.

 


PIC 2. Meneja wa SR FM Bw. Prosper Kwigize (Katikati) akitambulisha baadhi ya wafanyakazi wa standard radio kwa mgeni kutoka BBC Media Action.  Kulia kwake ni mtangazaji na mwandaaji wa vipindi Bw. Cales Katemana na kushoto kwake ni fundi mitambo wa SR Bw. Moses Anthony.

 

 PIC 3. Mtafiti kutoka BBC Media Action Bi. Matama (aliyeinama kulia) akisikiliza kwa makini majina ya wafanyakazi wa SR bali pia kutaka kujua kila mmoja anafananaje,  wakati wakitambulisha kwake. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa SR. Bw. James Daud.

Saturday, May 18, 2013

WASOMI KUTOKA KIGOMA WALIA NA WABUNGE WAO



Wabunge wa mkoa wa Kigoma wamehimizwa kujenga umoja na kuwa na mkakati maalumu wa kuutetea mkoa wa Kigoma na kuepuka ushabiki wa kisiasa ambao unatajwa kuiangamiza Tanzania
 
 
 
Raia hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Amos Nyandwi (pichani hapo juu) mchumi kutoka wizara ya kazi na ajira ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma katika kongamano la vijana wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini ambao ni wazawa wa Kigoma
 
Bw. Nyandwi amebainisha kuwa kwa sasa wabunge wote wa majimbo na viti maalumu kutoka mkoa wa kigoma  hawajaonesha umahili wao katika kubuni na kusimamia mipango ya maendeleo kwa njia ya umoja kama wawakilishi wa wanakigoma Bungeni
 
Amesisitiza kuwa licha ya kuwepo na wataalam walioajiliwa serikalini na katika sekta binafsi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisaidia kuchochea wabunge hao kuungana na kuwatumia wataalamu kuibua na kusimamia maendeleo lakini hakuna mwitikio wa wabunge hao
 
Aidha Nyandwi ameonya juu ya wanasiasa kung’ang’ana na vyma vya siasa na kushindwa kusimamia maslahi ya wananchi ambao ndio waliowapigia kura
 
Pamoja na lawama hizo kwa wabunge na wanasiasa, mchumi huyo amewahimiza wasomi walioko katika vyuo kufikiri kurejea mkoani Kigoma na kuunda au kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ii kunufaika na mipango ya serikali ya uwezeshaji jamii kiuchumi.
 
 
 
Kwa upande wake mkurugenzi wa makampuni ya Buhanzo na Standard Voice limited Bw. James Japhet (pichani hapo juu) amewaonya wasomi kutoka Kigoma kuondoa fikra za kutaka kuajiriwa badala yake wasome kwa umakini na watumie alimu yao kwa ajili ya ujasiriamali
 
Bw. Japhet ameongeza kuwa mkoa wa Kigoma una vyanzo vingi vya uchumi ambavyo havijatumika kuwainua wakazi wa mkkoa wa Kigoma hususani mazao ya ziwa Tanganyika, kilimo, ufugaji na fursa za biashara katika mipaka ya nchi jirani za Burundi, DRC na Zambia.
 
Aidha Bw. Japhet amewataka wabunge wa mkoa wa Kigoma kuungana pamoja kutetea ujenzi wa barabara pamoja na mkoa kuunganishwa na umeme wa gridi ya taifa, na kwamba bila miundombinu ya umeme na barabara za uhakika Kigoma haitapata maendeleo endelevu.
 
 
Zaidi ya wanafunzi 80 kutoka vyuo vya SAUT, Udom, SUA, Mzumbe, St. John, RUAHA na Tumaini wamehudhuria kongamano hilo, ambapo ni mbunge mmoja tu kutoka jimbo la Muhambwe Bw. Felix Mkosamali (pichani aliyekaa katikati juu) aliyejitokeza kushiriki.

Tuesday, May 7, 2013

MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AZURU MKOA WA SINGIDA

MAKAMU wa kwanza wa Rais, Serikali ya mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamadi amewataka Watanzania kudumisha upendo baina yao ili kuepuka chuki zinazoanza kujitokeza sasa nchini, kiasi cha kusababisha vurugu na vifo kwa wananchi wasiyo na hatia.
Maalimu Seif amesema hayo mjini Singida, kwenye ziara yake ya siku mbili mkoani humo iliyoanza May 06 2013 ambapo alipokelewa na viongozi wa serikali na chama cha wananchi CUF mkoani humo.
katika hotuba yake Bw. Seif amesema Watanzania siku zote wamekuwa ni watu wa amani, lakini vurugu zinazoanza kujitokeza sasa siyo za kistaarabu na zinaashiria kuna watu wanaochochea ili kufanikisha malengo waliyokusudia.
Alitumia fursa hiyo kuitaka serikali ya Tanzania kufuatilia kwa makini tukio la ulipuaji bomu katika ibada ya ufunguzi wa kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph mkoani Arusha, ili waliohusika wote wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
PICHA: Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mlozi akimkaribisha jukwaani Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ili kumpa fursa ya kuhutubia umati wa wananchi mjini Singida
 
Aidha alilaani shanbulio hilo la bomu kuiomba Serikali iendelee kulinda usalama wa wananchi wake kwa ajili ya kuenzi misingi imara ya amani, umoja na upendo iliyoasisiwa na waazilishi wa  Taifa la Tanzania.
Makamu wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad alimaliza ziara yake jana na alitarajiwa kuondoka mkoani Singida ili kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.