Wabunge wa mkoa wa Kigoma wamehimizwa kujenga umoja na kuwa
na mkakati maalumu wa kuutetea mkoa wa Kigoma na kuepuka ushabiki wa kisiasa
ambao unatajwa kuiangamiza Tanzania
Raia hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Amos Nyandwi (pichani hapo juu) mchumi
kutoka wizara ya kazi na ajira ambaye pia ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma katika
kongamano la vijana wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini ambao ni wazawa wa
Kigoma
Bw. Nyandwi amebainisha kuwa kwa sasa wabunge wote wa majimbo
na viti maalumu kutoka mkoa wa kigoma hawajaonesha
umahili wao katika kubuni na kusimamia mipango ya maendeleo kwa njia ya umoja
kama wawakilishi wa wanakigoma Bungeni
Amesisitiza kuwa licha ya kuwepo na wataalam walioajiliwa
serikalini na katika sekta binafsi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisaidia
kuchochea wabunge hao kuungana na kuwatumia wataalamu kuibua na kusimamia
maendeleo lakini hakuna mwitikio wa wabunge hao
Aidha Nyandwi ameonya juu ya wanasiasa kung’ang’ana na vyma
vya siasa na kushindwa kusimamia maslahi ya wananchi ambao ndio waliowapigia
kura
Pamoja na lawama hizo kwa wabunge na wanasiasa, mchumi huyo
amewahimiza wasomi walioko katika vyuo kufikiri kurejea mkoani Kigoma na kuunda
au kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ii kunufaika na mipango ya serikali ya
uwezeshaji jamii kiuchumi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa makampuni ya Buhanzo na Standard
Voice limited Bw. James Japhet (pichani hapo juu) amewaonya wasomi kutoka Kigoma kuondoa fikra za
kutaka kuajiriwa badala yake wasome kwa umakini na watumie alimu yao kwa ajili
ya ujasiriamali
Bw. Japhet ameongeza kuwa mkoa wa Kigoma una vyanzo vingi vya
uchumi ambavyo havijatumika kuwainua wakazi wa mkkoa wa Kigoma hususani mazao
ya ziwa Tanganyika, kilimo, ufugaji na fursa za biashara katika mipaka ya nchi
jirani za Burundi, DRC na Zambia.
Aidha Bw. Japhet amewataka wabunge wa mkoa wa Kigoma kuungana
pamoja kutetea ujenzi wa barabara pamoja na mkoa kuunganishwa na umeme wa gridi
ya taifa, na kwamba bila miundombinu ya umeme na barabara za uhakika Kigoma
haitapata maendeleo endelevu.
Zaidi ya wanafunzi 80 kutoka vyuo vya SAUT, Udom, SUA,
Mzumbe, St. John, RUAHA na Tumaini wamehudhuria kongamano hilo, ambapo ni mbunge mmoja tu kutoka jimbo la Muhambwe Bw. Felix Mkosamali (pichani aliyekaa katikati juu) aliyejitokeza kushiriki.
No comments:
Post a Comment