Maalimu Seif amesema hayo mjini Singida, kwenye
ziara yake ya siku mbili mkoani humo iliyoanza May 06 2013 ambapo alipokelewa na viongozi wa serikali na chama cha wananchi CUF mkoani humo.
katika hotuba yake Bw. Seif amesema Watanzania siku zote wamekuwa ni watu wa amani,
lakini vurugu zinazoanza kujitokeza sasa siyo za kistaarabu na zinaashiria kuna
watu wanaochochea ili kufanikisha malengo waliyokusudia.
Alitumia fursa hiyo kuitaka serikali ya Tanzania
kufuatilia kwa makini tukio la ulipuaji bomu katika ibada ya ufunguzi wa kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph mkoani Arusha, ili waliohusika
wote wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
PICHA: Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Queen Mlozi akimkaribisha jukwaani Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ili kumpa fursa ya kuhutubia umati wa wananchi mjini Singida
Aidha alilaani shanbulio hilo la bomu kuiomba Serikali
iendelee kulinda usalama wa wananchi wake kwa ajili ya kuenzi misingi imara ya
amani, umoja na upendo iliyoasisiwa na waazilishi wa Taifa la
Tanzania.
Makamu wa kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad alimaliza
ziara yake jana na alitarajiwa kuondoka mkoani Singida ili kuendelea na majukumu
mengine ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment