Na Boniface Mpagape.
Standard Radio FM iliyopo mjini
Singida, imeanza mchakato wa kushirikiana na Shirika la
utangazaji la Uingereza BBC katika kurusha baadhi ya vipindi na matangazo
kutoka shirika hilo.
Hali hiyo imedhihirika baada ya
Shirika la BBC Media Action kutuma afisa utafiti wake Bi. Suzy Matamwa ambaye
kulingana na maelezo yake mbele ya watumishi wa Standard radio atakuwa na
mazungumzo ya ana kwa ana na kila mwandishi kuhusiana na shughuli za kila siku
zinazofanyika katika masuala mbali mbali ya uandaaji wa habari na vipindi mbalimbali.
PIC 1. Bi. Suzy Matama akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Standard Radio katika ofisi za SR FM. Kutoka
kulia ni Meneja wa SR Bw. Prosper Kwigize, Mkurugenzi wa SR Bw. James Daud na
Bi. Suzy Matama kutoka BBC Media Action, wakati akitambulishwa rasmi.
Naye meneja wa Standard radio Bw. Prosper Kwigize amesema
kuwa Standard radio inatangaza vipindi mbali mbali vinavyoigusa jamii moja kwa
moja katika nyanja mbali mbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo, uchumi, ambavyo
hutangazwa na redio hiyo.
Aidha amesema standard radio imekuwa ikipokea wanafunzi
kutoka vyuo mbali mbali vya uandishi wa habari hapa nchini.
Amesema hivi sasa
kuna wanafunzi wanne waliopo katika mafunzo kazini na kwamba wengine
waliokuwepo wamemaliza muda wao na kurejea kwao na kwamba zaidi ya wanafunzi watango kutoka chuo kikuu cha mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza wanatarajia kuanza mafunzo kwa vitendo ndani ya Standard radio hivi karibuni
Afisa utafiti huyo kutoka shirika la BBC Media Action, amesema atakuwa akizungumza na wafanyakazi wa standard radio kwa nyakati tofauti kwa muda wa siku tatu, kuhusu masuala ya kawaida kama uandaaji wa vipindi, habari na kurusha matangazo kwa ujumla.
Endapo mpango huo utafanikiwa
itakuwa ni fursa nzuri kwa wakazi wa Singida kuweza kusikika katika ngazi ya
kimataifa kupitia BBC kwani nao pia watapata fursa ya kuchangia maoni
yao kuhusu masuala mbali mbali katika jamii.
Watumishi wa Standard radio pia
watanufaika kwa kupatiwa mafunzo pamoja na vitendea kazi ili kuwezesha ufanisi
katika kazi za kila siku za kuhabarisha na kuelimisha jamii.
PIC 2. Meneja wa SR FM Bw.
Prosper Kwigize (Katikati) akitambulisha baadhi ya wafanyakazi wa standard
radio kwa mgeni kutoka BBC Media Action.
Kulia kwake ni mtangazaji na mwandaaji wa vipindi Bw. Cales Katemana na
kushoto kwake ni fundi mitambo wa SR Bw. Moses Anthony.
PIC 3. Mtafiti kutoka BBC Media Action Bi. Matama (aliyeinama kulia) akisikiliza kwa makini majina ya wafanyakazi wa SR bali pia kutaka kujua kila mmoja anafananaje, wakati wakitambulisha kwake. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa SR. Bw. James Daud.
No comments:
Post a Comment