Sunday, May 5, 2013

MAALBINO WALINDWE NA KUTAMINIWA NA JAMII




Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw Pareseko Kone Ameshukuru Serikali na chama cha Walemavu wa ngozi Tanzania kwa kuupa heshima ya kuwa wenyeji wa maazimisho ya siku ya ualbino kitaifa  mkoa wa Singida.

 

Kauli hiyo imesema wakati wamaadhimisho ya siku ya Albino kitaifa yaliyofanyika jana katika uwanja wa  Namfua  Mkoani Singida.

 

Bw. Kone ameeleza kuwa wizara husika na chama cha walemavu wa ngozi Tanzania walijadili na kuamuwa kuwa Mkoa wa Singida ni moja kati ya mikoa inayoweza kuanda na kufanikisha shughuli hizo.


Aidha Bw Kone ameeleza kuwa kuwa kauli mbiu ya mwaka huu katika  maadhimisho hayo ni Kansa ya Ngozi Je Waijuwa, na mkoa wa wamejipanga kuhakikisha kuwa kila mlemavu wa ngozi anapata huduma iliyo ndani ya uwezo wa mkoa.

SIKU YA WALEMAVU WA NGOZI-ALBINO TANZANIA

Tuwalende na kuwajali wenye ulemavu




Wito Umetolewa kwa kila halmashauli ya Tanzania kuwa na bageti maalum kwa ilikuweza kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi kupata tiba kwa muda muafaka na kuwapatia huduma mbali mbali za kijamii

 

Kauliyo hiyo imesemwa na waziri wa tawala za mikoa na serikali za mitaa kutoka offisi ya waziri mkuu Bi. Hawa Ghasia katika kiwanja cha Namfua mkaoni Singida wakati wa maazimisho ya siku ya albino Kitaifa

 

Bi Hawa ameeleza kuwa  Halmashauli zinapaswa kufuatilia sensa iliyofanya ilikuweza kuwa na idadi kamili  ya watu hao ilikuweza kuwa na mgawanyo mzuri na utakao wawezesha wapeleka huduma kuwa na ufanisi wa kuwafikishia huduma kwa muda muafaka.

 

 

Aidha Bi Hawa amelani na kukemea Vitendo vya mauaji na kuwanyanya paa walemavu kuwa ni vitendo vya kikatili na atakaye bainika kufaya hivyo hatua kali za kisheria  zita chukuliwa.

 

 
 
 
 
 



Thursday, May 2, 2013

BONANZA LA STANDARD RADIO MEI MOSI 2013- MATUKIO KATIKA PICHA

Timu ya soka ya Standard Radio katika picha ya pamoja kabla ya mechi kati yao na mashabiki na wapenzi wa radio hiyo ijulikanayo kama STANDARD RADIO SALAAM CLUB FC muda mfupi kabla ya kuanza kwa mpambano ambao hata hivyo hakukuwa na mbabe baada ya timu zote kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja, mpambano huo ulichezwa katika uwanja wa ufukwe wa Ziwa Kindai mjini SIngida
 
 
Meneja wa Standard Radio Bw. Prosper Kwigize akisikilliza maelekezo ya kocha muda mfupi kabla ya mechi kuanza, Kwigize kutoka winga ya kulia ndiye aliyetoa pasi iliyosababisha kupatikana kwa bao la kusawazisha kipindi cha pili, mbele aliyeshika nyonga ni mchezaji centre half Imani Msigwa



























Kikosi cha Standard Radio FC kikijipanga kuzuia mpira wa adhabu kutoka kwa wapinzani wake STANDARD salaam club FC, Mwenye jezi namba 13 mgongoni ni mwanaspoti wetu Cales Katemana na jezi namba 12 ni Abdul Bandola  mtayarishaji msaidizi wa kipindi cha Michezo kinachorushwa na standard radio kila siku saa moja na nusu jioni



























Abdul Bandola (kulia menye bukta ya njano) star wa Standard Radio fc akichapa mwendo kufunga bao la ushindi, hata hivyo walinda mlango wa Salaam Club FC walifanikiwa kuzuia mashambulizi.

Meneja wa Standard Radio akiongoza kikosi cha mashabikii na watangazaji kuelekea uwanjani tayari kwa mtifuano wa Bonanza la Standard radio na Mei Mosi, Standard Radio Imeahidi kuendesha matamasha mbalimbali pamoja na mashindano ya soka kwa wanaume na wanawake kama sehemu ya kuitangaza Radio hiyo, Hivi karibuni lilifanyika tamasha kubwa na zuri wilayani Ikungi na inatarajiwa kufanyika tena mjini Singida na Iramba kabla ya kuenlekea Igunga na Nzega mkoani Taboba na baadaye matamasha hayo yatafanyika katika wilaya za Hanang na Mbulu mkoani Manyara

Bw. Boniface Mpagape (mwenye koti) ambaye ni Mhariri wa Standard Radio ambaye ni Mhariri akiongoza kikosi cha pili cha soka kutoka SR FM kuelekea uwanjani muda mfupi kabla ya mechi hiyo kuanza, Mpagape a.k.a Furgason) ndiye Kocha mchezaji wa timu ya soka ya Standard Radio

Wednesday, May 1, 2013

HELVETAS USWISS YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA STANDARD RADIO

Maafisa wa shirika la maendeleo la Uswiss wakizuru ofisi na jumba la matangazo la Standard Radio mkoani Singida katika ziara yao maalumu ya kutembelea kituoo hicho kwa malengo ya kuandaa mkakati wa kuanzisha ushirikiano katika kuandaa vipindi vya maendeleo hususani katika kilimo na ufugaji

katika kipicha kutoka kushoto Bw. Christian Bobst mpiga picha kutoka nchini Uswiss, Bi. Astrid Rana na Bi. Franca Palmy maafisa wa Helvetas wanaohusika na masuala ua ushirikiano na utunishaji wa mfuko wa maendeleo kwa ukanda wa Afrika na mwenye suti nyeusi ni Bw. Prosper Kwigize Meneja wa Standard Radio

katika picha ni Bw. Yusuph Salum mratibu wa shirika la Helvetas mkoanii Singida akiwa na Maafisa wake kutoka nchini Uswiss katika studio za Standard Radio, walikuwa wakishuhudia mafumo wa matangazo na namna matangazo yanavyorushwa na mtangazazji wa zamu