Tuesday, March 5, 2013

WATUMA SALAAM SINGIDA NA UBUNIFU WA AINA YAKE

Baadhi ya kadi zilizoundwa na watuma salaam baada ya kukosa kadi harali za STANDARD RADIO katika maeneo yao

Ujio wa Standard Radio fm mkoani Singida, imekuwa kama ukombozi wa aina yake, viashiria vingingi vimethibitisha kuwa Standard radio imepokelewa na wanasingida na mikoa ya jirani kwa mikono miwili.

 

Vipindi vyake murua vimekuwa kivutio na kiunganishi muhimu kwa wananchi na viongozi wao, lakini pia kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya jamii kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kijamii

 

Baadhi ya kipindi cha Salaam kwa njia ya kadi kuanza kila kona watu wamezisaka na pale walipozikosa waliamua kubuni namna ya kupata kadi hizo na kuzifikisha Studio ili salaam zao zisome.

 

Pichani hapo juu ni ubunifu uliofanywa na baadhi ya watuma salaam na wapenzi wa standard Radio mkoani Singida, Tabora, Dodoma na Manyara

Pichani, Ni kadi harali za standard radio zikiwa zimejazwa na wasikilizaji wa kipindi cha salaam

HABARI KUTOKA STANDARD RADIO


MANYONI

Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bw Mizengo Peter Pinda Leo Amezindua Rasim Siku Ya Maadhimisho Ya Siku Ya Utundikaji Mizinga Ili Mananchi Wapate Elimu Ya Ufugaji Nyuki Katika Kijiji Cha Agondi Wilayani Manyoni

 

Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania katika ziara ya maadhimisho ya kitaifa ya siku ya utundikaji mizinga wilayani manyoni katika mkoa wa singida.

Katika uzinduzi huo pinda amesema zao la asali limetajwa katika vitabu vitakatifu kama bibilia na quruan na kwamba asali ni dawa kutokana na virutubisho vyake bali pia ni chakula.

Aidha pinda amezungumzia kuhusu mikakati iliyopo kutoka wizarani kwamba serikali imeongeza udahili wa wanafunzi katika chuo cha nyuki cha tabora  kutokia wanafunzi 98 hadi kufikia 120 katika chuo hicho.

Katika ziara hiyo waziri mkuu amefwatana na baadhi ya viongozi wa serikali ambao ni waziri wa uwekezaji,kutoka ofisi ya waziri mkuu bi merry nagu na wakuu wa mikoa jirani ya arusha, dodoma na simiyu.

 

 

TABORA

Mchakato wa uundwaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Sikonge uko mbioni kukamilika baada ya kamati ndogo iliyoundwa kuwa katika hatua za mwisho.

Akisoma taarifa yake mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mwishoni mwa wiki, mwanasheria wa halmashauri hiyo, Richard Unambwe, amesema tayari kamati yake ilifanya ziara ya kujifunza katika mikoa ya Mbeya na Iringa.

Unambwe ameongeza kuwa mamlaka ya mji mdogo wa Sikonge kwa taratibu zilivyo,  utahusisha vijiji vya Sikonge, Mlogolo, Mwamayunga, Kisanga, Mkolye na Igalula.

Aidha, amesema kuwa hatua nyingine za uanzishwaji zimezingatia uwepo wa ramani inayoonesha mipaka ya mamlaka ya mji husika, maelezo ya utambuzi wa mipaka hiyo kwa kushirikisha vijiji hivyo, ikiwemo ukubwa wa eneo lililotengwa kwa ajili ya kuchukuliwa na mamlaka.

Akihitimisha mjadala huo Unambwe amesema,  hatua nyingine ni kuwepo utayarishaji wa taarifa ya mchanganuo wa matumizi mbalimbali ya ardhi iliyochukuliwa pamoja na vyanzo vya mapato, ikiwemo eneo la makazi, viwanda, taasisi na barabara.

 

 

 

 

DAR ES SALAAM

Rais mtaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, ameionya jamii ya Kitanzania kuwa makini na watu wanaochochea masuala ya udini.

Mwinyi alitoa wito huo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Polisi Mess Msasani, wakati wa uzinduzi wa kipindi cha ‘Pamoja Tunaweza’ kilichobuniwa na Terry Gbemudu maarufu kwa jina la Mama Terry na kuongeza kuwa ni vema kila Mtanzania akajishugulisha na utunzaji wa amani iliyopo, kwani hali ya nchi inakoelekea ni kubaya.

Hata hivyo, ameonya jamii kuwa makini na vurugu za kidini, hasa mauaji ya viongozi wa dini kwani limekuwa suala linalohatarisha amani ya nchi, hivyo ni jukumu la kila mtu kuchukua tahadhari.

Aidha Mwinyi amesema ni vema jukumu la kulea watoto likawa la kila mmoja wetu, kwani hivi sasa kila mtu amekuwa akishughulika na famila yake pekee, jambo ambalo ni hatari kwa siku zijazo kwa watoto wasio kuwa na walezi, wamekuwa hawapati malezi yanayostahili kutoka kwenye jamii.

Kipindi hicho cha televisheni kitakachokuwa kinaelimisha jamii juu ya kupamba na dawa za kulevya, kinatarajiwa kuanza kurushwa na Shikika la Utangazaji Nchini (TBC) kila Jumatatu.

 

 

 

 

SINGIDA

Mwenyekiti wa jumuhiya ya wazazi CCM wilaya ya Ikungi Bw Shabani Hassani Mtakii amewataka watendaji wa vijiji kuwajibika na kuwa na nidhamu katika fedha zinachochangwa na wananchi ili kuepusha migogoro iliyopo kati ya wananchi na serikali kwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi ili waweze kujua kupanga vizuri mikakati yao ya maendeleo.

Mtakii ameyasema hayo mwishoni mwa juma katika kijiji cha Mtunduru kata ya Mtunduru wilaya ya Ikungi baada ya kutembelea, kukagua na kuhoji matatizo yaliyosababisha kutomalizika  kwa shule hiyo mpya ya kitongoji cha Mtakuja inayojengwa kwa nguvu za wananchi tangu ianze ujenzi wake mwaka 2000 ambapo hadi sasa ni darasa moja tu limejengwa na ofisi moja ya waalimu huku michango ikitolewa kila mwaka na hakuna maendeleleo ya shule hiyo.

Amesema wananchi wanayo haki ya kudai taarifa za michango yao ya shule inayotumika, na kuhoji taarfa za michango hiyo ilivyotumika na inavyotumika hivyo ni wajibu wa watendaji wa vijiji kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi kama katiba inavyoelekeza, ili kuondoa sintofahamu kati ya wananchi na serikali katika fedha wanazochangia miradi.

Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Ikungi Bw Daud Kapambala amesema lengo la mwenyekiti wa jumuiya hiyo kutembelea shule hiyo ni kukagua, kupokea kero za wananchi na kuhoji matatizo ya kutomalizika kwa shue hiyo      

Friday, March 1, 2013

SILAHA ZAKAMATWA MKOANI SINGIDA


SINGIDA

Jeshi la polisi na kwa kushirikiana na askari wa misitu wilayani Manyoni Mkoani Singida,  limefanikiwa kukamata zaidi ya  risasi mia mbili na bunduki tatu za magobore.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Singida Bw Linus Sinzumwa amesema hay oleo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake.

Bw. Sinzumwa amesema kuwa jana majira ya saa kumi na moja asubuhi jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari wa misitu wamefanikiwa kukamata risasi na bunduki aina ya magobore katika kijiji cha Sapapa katika tarafa ya Itigi wilayani Manyoni Mkoani Singida. Amesema risasi hizo zinatumika katika bunduki aina ya SMG.

 
Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani humo ametoa wito kwa raia kutoa taarifa kwa askari ili kuweza kukabilina na vitendo vya kihalifu vinayoendelea kutokea kwani ni njia mbadala ya kukomesha uhalifu.

MH. PINDA KUZINDUA UTUNDIKAJI MIZINGA YA NYUKI KITAIFA MKOANI SINGIDA

Na. Boniface Mpagape     

Serikali kupitia wizara ya maliasili na Utalii imeanzisha siku ya utundikaji mizinga kitaifa mwaka huu, kwa lengo la kuongeza msukumo katika sekta hiyo yenye uwezo wa kuondoa umaskini.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone kwa vyombo vya habari leo, imesema uzinduzi wa mkakati huo kitaifa utafanyika Machi 4, wilayani Manyoni mkoani Singida na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Mizengo Peter Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

 

Dk. Kone amesema hii ni heshima kubwa kwa mkoa wa Singida na wananchi wake na ni heshima kwa wafuga nyuki wote wa mkoa wa Singida.

 

Amesema ufugaji nyuki ni njia sahihi ya kutumia raslimali za misitu katika kujiongezea kipato, badala ya kuharibu mazingira kwa kukata miti ili kuchoma mkaa kwani ufugaji huo unatunza miti kwa sababu ni chanzo kikuu cha asali.

 

Amewataka wananchi wa mkoa wa Singida kutumia fursa hiyo kwa kuongeza idadi ya mizinga katika mashamba yao, na wale ambao hawajaanza waanze leo. Mkuu wa mkoa wa Singida ametoa ushauri kujiwekea lengo la kutundika mizinga angalau mitano kila mwaka.

 

Aidha, amewaomba wananchi wote siku ya tarehe 4 Machi mwaka huu, kujitokeza kwa wingi katika hifadhi ya nyuki ya Aghondi wilayani Manyoni, ili kushuhudia uzinduzi na kujifunza mbinu mbali mbali za kisasa za ufugaji nyuki.

 

Kauli mbiu ya siku ya taifa ya utundikaji mizinga mwaka huu, ni Fuga nyuki uongeze kipato, tundika mizinga.