MANYONI
Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bw
Mizengo Peter Pinda Leo Amezindua Rasim Siku Ya Maadhimisho Ya Siku Ya
Utundikaji Mizinga Ili Mananchi Wapate Elimu Ya Ufugaji Nyuki Katika Kijiji Cha
Agondi Wilayani Manyoni
Hayo
yamesemwa na waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania katika ziara ya maadhimisho
ya kitaifa ya siku ya utundikaji mizinga wilayani manyoni katika mkoa wa
singida.
Katika
uzinduzi huo pinda amesema zao la asali limetajwa katika vitabu vitakatifu kama
bibilia na quruan na kwamba asali ni dawa kutokana na virutubisho vyake bali
pia ni chakula.
Aidha
pinda amezungumzia kuhusu mikakati iliyopo kutoka wizarani kwamba serikali
imeongeza udahili wa wanafunzi katika chuo cha nyuki cha tabora kutokia wanafunzi 98 hadi kufikia 120 katika
chuo hicho.
Katika
ziara hiyo waziri mkuu amefwatana na baadhi ya viongozi wa serikali ambao ni
waziri wa uwekezaji,kutoka ofisi ya waziri mkuu bi merry nagu na wakuu wa mikoa
jirani ya arusha, dodoma na simiyu.
TABORA
Mchakato wa uundwaji wa
mamlaka ya mji mdogo wa Sikonge uko mbioni kukamilika baada ya kamati ndogo
iliyoundwa kuwa katika hatua za mwisho.
Akisoma taarifa yake
mbele ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mwishoni mwa
wiki, mwanasheria wa halmashauri hiyo, Richard Unambwe, amesema tayari kamati
yake ilifanya ziara ya kujifunza katika mikoa ya Mbeya na Iringa.
Unambwe ameongeza kuwa
mamlaka ya mji mdogo wa Sikonge kwa taratibu zilivyo, utahusisha vijiji vya Sikonge, Mlogolo,
Mwamayunga, Kisanga, Mkolye na Igalula.
Aidha, amesema kuwa
hatua nyingine za uanzishwaji zimezingatia uwepo wa ramani inayoonesha mipaka
ya mamlaka ya mji husika, maelezo ya utambuzi wa mipaka hiyo kwa kushirikisha
vijiji hivyo, ikiwemo ukubwa wa eneo lililotengwa kwa ajili ya kuchukuliwa na
mamlaka.
Akihitimisha mjadala
huo Unambwe amesema, hatua nyingine ni
kuwepo utayarishaji wa taarifa ya mchanganuo wa matumizi mbalimbali ya ardhi
iliyochukuliwa pamoja na vyanzo vya mapato, ikiwemo eneo la makazi, viwanda, taasisi
na barabara.
DAR ES SALAAM
Rais mtaafu wa Awamu ya
Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, ameionya jamii ya Kitanzania kuwa makini na
watu wanaochochea masuala ya udini.
Mwinyi alitoa wito huo
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Polisi Mess Msasani,
wakati wa uzinduzi wa kipindi cha ‘Pamoja Tunaweza’ kilichobuniwa na Terry
Gbemudu maarufu kwa jina la Mama Terry na kuongeza kuwa ni vema kila Mtanzania
akajishugulisha na utunzaji wa amani iliyopo, kwani hali ya nchi inakoelekea ni
kubaya.
Hata hivyo, ameonya
jamii kuwa makini na vurugu za kidini, hasa mauaji ya viongozi wa dini kwani
limekuwa suala linalohatarisha amani ya nchi, hivyo ni jukumu la kila mtu
kuchukua tahadhari.
Aidha Mwinyi amesema ni
vema jukumu la kulea watoto likawa la kila mmoja wetu, kwani hivi sasa kila mtu
amekuwa akishughulika na famila yake pekee, jambo ambalo ni hatari kwa siku
zijazo kwa watoto wasio kuwa na walezi, wamekuwa hawapati malezi yanayostahili
kutoka kwenye jamii.
Kipindi hicho cha
televisheni kitakachokuwa kinaelimisha jamii juu ya kupamba na dawa za kulevya,
kinatarajiwa kuanza kurushwa na Shikika la Utangazaji Nchini (TBC) kila
Jumatatu.
SINGIDA
Mwenyekiti wa jumuhiya ya wazazi CCM wilaya ya
Ikungi Bw Shabani Hassani Mtakii amewataka watendaji wa vijiji kuwajibika na
kuwa na nidhamu katika fedha zinachochangwa na wananchi ili kuepusha migogoro
iliyopo kati ya wananchi na serikali kwa kuwasomea wananchi mapato na matumizi
ili waweze kujua kupanga vizuri mikakati yao ya maendeleo.
Mtakii ameyasema hayo mwishoni mwa juma katika
kijiji cha Mtunduru kata ya Mtunduru wilaya ya Ikungi baada ya kutembelea,
kukagua na kuhoji matatizo yaliyosababisha kutomalizika kwa shule hiyo mpya ya kitongoji cha Mtakuja
inayojengwa kwa nguvu za wananchi tangu ianze ujenzi wake mwaka 2000 ambapo
hadi sasa ni darasa moja tu limejengwa na ofisi moja ya waalimu huku michango
ikitolewa kila mwaka na hakuna maendeleleo ya shule hiyo.
Amesema wananchi wanayo haki ya kudai taarifa
za michango yao ya shule inayotumika, na kuhoji taarfa za michango hiyo
ilivyotumika na inavyotumika hivyo ni wajibu wa watendaji wa vijiji kuwasomea
wananchi taarifa za mapato na matumizi kama katiba inavyoelekeza, ili kuondoa
sintofahamu kati ya wananchi na serikali katika fedha wanazochangia miradi.
Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya wazazi
wilaya ya Ikungi Bw Daud Kapambala amesema lengo la mwenyekiti wa jumuiya hiyo
kutembelea shule hiyo ni kukagua, kupokea kero za wananchi na kuhoji matatizo
ya kutomalizika kwa shue hiyo
No comments:
Post a Comment