Ajenda ya Maendeleo Baada-ya-2015 na Mustakabali
wa Nishati Tunaoutaka kwa Wote
Tanzania, Norway na Umoja wa Mataifa washirikiana
mjadala wa ajenda ya nishati
Dar es Salaam, Machi 18— Wakati mwaka 2015
unakaribia kwa kasi, bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuharakisha kufikiwa kwa
Malengo ya Milenia. Wakati huo huo, tunatakiwa tuanze kufikiria nini kitafuata
baada ya mwaka 2015. Mjadala huu tayari umeshaanza, kama ilivyoonekana wakati
wa “Rio+20”, na serikali katika miaka inayokuja zitajadili na kuamua ajenda ya
maendeleo baada-ya-2015.
Katika kuchangia
majadiliano haya, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa
kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania wamewezesha,
na kwa pamoja wanakuwa wenyeji wa mchakato wa mjadala wa wazi wa kanda Afrika
ukihusisha makundi mbalimbali yenye maslahi ikiwamo serikali, asasi za kiraia,
sekta binafsi, wasomi na vijana, kuelewa changamoto na fursa zao, na jinsi ya
kuingiza masuala ya nishati kwenye ajenda ya maendeleo baada-ya-2015. Ripoti
kutoka kwenye mashauriano haya itatoa mchango mzuri kwenye mkutano unaopangwa
kufanyika katika ngazi ya kimataifa.
Nishati ni suala muhimu katika
juhudi za kimataifa kushawishi mabadiliko ya dhana kuelekea kwenye kuondoa
umaskini, shughuli za kiuchumi zinazojali mazingira na hatimaye maendeleo
endelevu. Kwa namna mbalimbali, mjadala wa kimataifa kuhusu nishati na
maendeleo endelevu tayari umeshaanza. Miaka mitano iliyopita imeshuhudia
kuongezeka kwa shauku kuhusu masuala ya nishati, ikianza na tamko la Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa kuutaja mwaka 2012 kama “Mwaka wa Kimataifa wa Nishati
Endelevu kwa Wote”. Kwa kutambua umuhimu na uharaka wa changamoto za nishati,
viongozi katika serikali, biashara na asasi za kiraia wanahitaji kujenga uelewa
kimataifa juu ya umuhimu wa nishati kwa maendeleo endelevu.
Katika mchakato wa
kuhusisha wadau kuhusu hayo yaliyoelezwa, mkutano wa majadiliamo umepangwa
kufanyika tarehe 19 Machi 2013 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
Salaam. Watoa mada wakuu mbalimbali
akiwemo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa; Mkurugenzi wa Nishati, Mazingira na
Mabadiliko ya Tabia Nchi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na Waziri wa
Ushirikiano wa Kimataifa wa Norway wamealikwa. Mkutano huu utafunguliwa na
Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo.
Masuala muhimu
yatakayojadiliwa wakati wa mkutano ni pamoja na : Upatikanaji wa Nishati kwa
Wote; Kuongezeka kwa Ufanisi na matumizi endelevu ya Nishati.
Wadau wote wa nishati
wanakaribishwa katika mkutano huu.
Kwa
Taarifa Zaidi Wasiliana na:
Mr Geir Yngve Hermansen, Norwegian Embassy geir.yngve.hermansen@mfa.no
No comments:
Post a Comment