SINGIDA
Kamati ya bunge tawala za mikoa na
serikali za mitaa imeitaka serikali kupitia ofisi ya mkaguzi wa hesabu za
serikali kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha zilizotumika kujenga
kibanda cha kuchomea taka katika hospitali mpya ya rufaa mkoani Singida.
Akitoa maazimio ya kamati hiyo mara
baada ya kupokea taarifa fupi kuhusu ujenzi wa hospitali mpya ya rufaa ya mkoa
wa singiga leo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk Hamisi Kigwangara amesema kibanda
hicho, kinaonyesha kugharimu milioni 98 na nne jambo ambalo sio sahihi
ikilinganishwa na gharama halisi mara baada ya kuona mradi huo.
Amesema mkataba wa ujenzi unaonyesha
kuwa bati zilizotumika katika ujenzi zinagharimu milioni kumi huku kukiwa
hakuna uhalisia kati ya idadi ya bati na fedha iliyotumika jambo linaloonyesha mapungufu
Aidha amesema serikali inatakiwa
kutuma fedha za kukamilisha mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ambazo
zilipitishwa katika bunge takribani bilioni mbili ili kuharakisha ujezi wa
hospitali hiyo
Kamati hiyo ya bunge imefanya ziara
ya siku mbili mkoani Singida ambapo imekagua miradi pamoja na kuzungumza na
sekretarieti ya mkoa na imerejea leo mjini Dodoma
Source: SR/Hawa
Ed: BM
Date;21/3/2013
SINGIDA
Jumla ya wahamiaji haramu 30 wameripotiwa kuingia mkoani
Singida kwa kipindi cha January 2012
hadi march 2013 kinyume cha sheria.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari afisa uhamiaji mkoa wa
Singida
Bw.Adam Mnyeke amesema wahamiaji hao wanatoka katika nchi za
Ethiopia,Somalia, Burundi na Kenya na kwamba hupita njia zisizo rasmi.
Amesema miongoni mwa wahamiaji hao waethiopia ni 24,wasomali
3, wakenya 2 na mrundi mmoja.
Aidha amesema uchunguzi umebaini chanzo cha wahamiaji hao
haramu kutoka katika nchi zao kuwenda nchi jirani ni kutokana na hali ngumu ya maisha, na hali
mbaya ya kiusalama katika nchi zao,na hufanya hivyo kunusuru maisha yao
Source: SR/Bandola
Ed: BM
Date;21/3/2013
SINGIDA
Wito umetolewa kwa wananchi kwa kushirikiana na vikundi vya
polisi jamii katika suala la kufanya usafi katika kata ya utemini ndani ya
manispaa ya Singida
Mtendaji wa kata hiyo
Bw. Noel Hago ametoa wito huo wakati akiongea na Standard Redio leo ofisini
kwake.
Bw. Hago amesema hayo kufuatia siku iliyopangwa na viongozi
kwa kushirikiana na polisi kata, kufanya
usafi siku ya tarehe 22 mwezi 3 mwaka huu.
Aidha Bw. Hago amesema wananchi wanapaswa kuonyesha ushirikiano
wao dhidi ya viongozi ili kuweza kufanikisha zoezi hilo.
Source: SR/Hawa
Ed: BM
Date;21/3/2013
SINGIDA
Chama cha wafanyabiashara, viwanda,na kilimo
mkoani singida TCCIA kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufu wa fedha na kukosa wafadhili.
Hayo yamesemwa na afisa mtendaji wa
chama hicho mkoani singida Bw. Calvert Nkurlu wakati akizungumza na standard
radio ofisini kwake.
Amesema chama hicho kilianzishwa kwa
lengo la kuunganisha nguvu ya wafanyabiashara, viwanda, pamoja na wakulima wawe
na sauti moja katika masuala yanayowahusu ili kuendesha biashara kwa ufanisi
Aidha chama mkoani Singida kina
wanachama mia sita themanini na sita, idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na
wafanyabiashara na wakulima waliopo katika mkoa wa singida
Ametoa wito kwa wafanya biashara kutumia
mitandao mbalimbali ili kupata habari zinazohusu biashara, kusajili majina ya biashara,
pamoja serikali kukaa pamoja na wafanyabiasha ili kujadili hali halisi ya
biashara
Source: Tanzania Daima
Source: Tanzania Daima
Ed: BM
Date;21/3/2013
BUKOBA
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa
ya Bukoba wamedai kuwa Meya wao, Anatory Amani, amekuwa akiendesha shughuli
zake kibabe, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha matumizi ya fedha bila
kuwashirikisha.
Madiwani hao wametoa madai hayo jana mbele ya tume iliyoundwa na
Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuchunguza tuhuma za
ufisadi wa miradi mitatu zinazomkabili meya huyo, ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Abbas Kandoro.
Wajumbe wengine mbali na Kandoro ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.
Rehema Nchimbi, Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi na Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali.
Madiwani hao kwa nyakati tofauti wameiambia tume kuwa Amani
amekuwa mbabe na kufikia hatua ya kuhamisha fedha kutoka mfuko wa mradi wa
viwanja sh milioni 200 kwenda kulipia deni la mradi wa soko bila idhini yao.
Source: SR/E. Lyatuu
Source: SR/E. Lyatuu
Ed: BM
Date;21/3/2013
SINGIDA
Wananchi wa kijiji cha Mandewa Kata
ya Mandewa manispaa ya Singida, wametakiwa kuwa na subira kuhusu suala la
kuhamishwa kwa soko la gineri
Mtendaji wa Kata hiyo Bw. Bakari
Ntandu amesema hayo wakati akizungumza na standard radio ofisini kwake, kuhusu
mikakati iliyopo ya kuhamishwa kwa soko hilo.
Amesema eneo linalotumika kama
soko, linatumika kwa muda na wala halikupangwa maalum kwa ajili ya soko na
kwamba lipo eneo husika kwa ajili hiyo na utaratibu wa kuhamia katika eneo hilo
unafanyika.
Amesema utaratibu unaofanyika ni
kusubiri kampuni ya Spencon kukamilisha mradi wa maji, kwa kuwa eneo
lililotengwa kwa ajili ya soko lipo karibu na mradi wa maji unaojengwa.
No comments:
Post a Comment