Source: SR/Neema J.
Ed: BM
Date: March 12, 2013.
Mtu
mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa
baada ya gari walilokuwa wakisafiria
kupinduka baada ya kutokea
hitilafu za kiufundi na kusababisha
ajali hiyo katika kijiji cha kisaki
tarafa ya mungu maji mkoani singida.
Kamanda
wa polisi mkoani Singida ACP Linus Sinzumwa amesema ajali hiyo imetokea jana
majira ya saa nne usiku katika barabara ya Singida kwenda Dodoma na kutaja
namba ya usajili ya gari hilo kuwa ni gari namba C 6017 aina ya Nissan presage.
Kamanda
Sinzumwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni
kutokana na rock hand na driving
shaft ya gari hilo kukatika hivyo kusababisha ajali na kumtaja
aliyefariki kuwa ni Abubakari Bukungukize ambaye ni mfanyabiashara wa Rwanda, na aliyepata ajali ni Vidal Ruse ambaye ni raia wa Sweden
Pia
amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida na
majeruhi bado anaendelea na matibabu na uchunguzi bado unaendelea kufanyika.
Amesema
bado wanaendelea kuwasiliana na ndugu zao ili waje kuchua maiti na majeruhi
huyo
Source:
SR/
Ed: BM
Date: March 12, 2013.
KASULU
Katibu
wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Bw.
Masud Kitowe ameuagiza uongozi wa kata ya shunguliba na kijiji cha malalo wilayani
humo kuhakikisha mafundi waliopewa kazi ya kujenga nyumba ya mwalimu katika shule
ya msingi malalo wanakamilisha ujenzi huo mara moja
Bw
Kitowe ameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji
cha malalo wilayani kasulu baada ya kufanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo katika kata ya shunguliba sambamabamba na kufanya ukaguzi juu ya utekewlezaji
wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi.
Bw
Kitowe amesema amepata taarifa kuwa mafundi waliopewa kazi ya kujenga nyumba hiyo
wamesimama kuendelea na ujenzi kwa kile kinachodaiwa kuwa mafundi wamekwenda katika
mashamba yao kulima. Amewaagiza viongozi hao kuhakikisha mafundi hao wanarejea na
kumalizia ujenzi huo mara moja
Aidha
Bw Kitowe amewataka viongozi hao kuhakikisha mafundi hao wanapatikana na kuendfelea
na ujenzi wa nyumba hiyo na kama itashindikana basi mafundi hao warejeshe pesa walizopewa
kwa ajili ya ujenzi huo na kuikabidhi kazi hiyo kwa mafundi wengine ili kukamilisha
ujenzi wa nyumba hiyo ya mwalimu shuleni hapo
Source: SR/E. LYATUU
Ed: BM
Date: March 12, 2013.
SINGIDA
Wananchi
Katika manispaa ya Singida wametakiwa kuwa
makini na utupaji ovyo wa taka
ili kuweka mji
safi na kuepukana
na magonjwa ya
mlipuko mkoani hapo
Bw. Seif Swedy,
afisa afya na mazingira wa
manispaa amesema hayo
wakati akizungumza na
standard redio ofisini
kwake.
Amesema kuwa endapo wananchi wataonyesha mwitikio kwa
kujituma kusafisha maeneo yao na kukusanya taka
sehemu moja, hakutakuwa na
magonjwa ya mlipuko kama vile
kipindupindu na badala
yake mji kuwa safi na swala la afya
kuwa katika usalama.
Hata
hivyo amesema chanzo cha
taka kuzagaa ni kutokana
na wananchi kutojali afya zao
kutokana na hana potofu waliojiwekea
kwa kuamini suala la usafi linahusika na manispaa, hivyo amewataka wananchi wawajibike katika kuweka mji katika
hali ya usafi.
Bw Seif
Swedy amewataka wananchi kuwa na mwamko wa kujali mazingira kuwa katika hali ya
usafi na kila mwananchi
kuwa mlinzi wa mwenzake, ili
kudhibiti tatizo la utupaji ovyo
wa taka na kufuta dhana ya
kutegemea manispaa kuhusika na
usafi katika mji
huo
Source: Tanzania Daima
Ed: BM
Date: March 12, 2013.
DAR
ES SALAAM
Vituo
vya televisheni vinavyomilikiwa na kampuni binafsi, viko hatarini kufungwa kutokana
na mfumo wa matangazo wa digitali kuathiri upatikanaji wa matangazo.
Vituo
vilivyopo kwenye hatari ya kufunga matangazo yao ni pamoja na ITV, Star TV,
Clouds TV, DTV na vingine binafsi.
Taarifa
za kufungwa kwa vituo hivyo, imetolewa jana na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Nchini MOAT upande wa televisheni, wakati wakizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa MOAT, Bw. Reginald Mengi, amesema vituo hivyo viko hatarini kufungwa kwani
idadi kubwa ya watumiaji wa televisheni imepungua kutokana na kukosa ving’amuzi
na hivyo kuathiri upatikanaji wa matangazo.
Bw. Mengi
amesema ili matangazo ya vituo vya televisheni yaendelee kupatikana, ameitaka
serikali irejeshe matangazo ya analojia sambamba na digitali ili kuwapa nafasi
watumiaji wa televisheni kujiandaa kuingia kwenye mfumo wa digitali.
Ameikosoa
serikali kwa kuingiza matangazo ya mfumo wa digitali haraka bila kutoa muda wa
kutosha kwa wananchi kujiandaa kwani haoni sababu ya Tanzania kuingia haraka
kwenye mfumo huo.
Naye
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, anayemiliki kituo cha
televisheni cha Clouds, amesema nusu ya matangazo kutoka kwa wateja wao
yameondolewa baada ya matangazo yao kutowafikia watu wengi.
Kwa
upande wake, Samuel Nyala, Mkurugenzi wa Sahara Media Group wamiliki wa kituo
cha Star TV, amesema baadhi ya mikoa iliyoanza kurusha matangazo ya digitali,
wamekwama kwani hakukuwa na maandalizi wakati mitambo ya analogia inazimwa.
Source: SR/Beatrice
Ed: BM
Date: March 12, 2013.
SINGIDA
Watu
watano wakazi wa manispaa ya Singida, wamefikishwa katika mahakama ya hakimu
mkazi, wakikabiliwa na shtaka la kuvunja na kuiba katika jengo la kampuni ya
vinywaji ya Bonite, eneo la Mwenge mjini Singida.
Akisoma
kesi hiyo mwendesha mashtaka, Bw. Mussa Chemu mbele ya hakimu mfawidhi wa
mahakama ya hakimu mkazi, Bi. Telsefia Tesha, washtakiwa hao wamekana mashtaka
dhidi yao.
Imeelezwa
kuwa February 18 mwaka huu, majira ya usiku maeneo ya Mwenge ulifanyika
uvunjaji huo na mali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na
tatu Mali ya kampuni ya Bonite.
Washtakiwa
hao watano ni walinzi wa kampuni hiyo, ambao ni Zabron Ibrahim mkazi wa Puma
Singida, Kautusi Francis mkazi wa Unyamikumbi Singida, Kassim Peter mkazi wa
Misinko Singida, wengine ni Ladislaus Masini mkazi wa kibaoni Singida na Musa
Gambuna mkazi wa kibaoni Singida.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi tarehe 26 mwezi huu itakapotajwa tena, na upelelezi bado
unaendelea kufanyika wakati washtakiwa wamerudishwa rumande.
Source:
SR/Matinde Nestory
Ed: BM
Date: March 12, 2013.
MWANZA
Meneja
Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka katika jiji la Mwanza Bw. Robert
Masunya amewataka wananchi kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya maji
yatakayofanyika wiki hii
Wito
huo umetolewa mapema hii leo wakati radio standard ilipokuwa ikifanya
mazungumzo ofisini kwake
Bw.Masunya
amesema kuwa maadhimisho hayo yatafanyika march 16 mwaka huu katika viwanja vya
Furahisha jijini Mwanza ambapo kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji ni march
22 mwaka huu.
Meneja
Uhusiano huyo amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu katika siku ya maji ni MWAKA WA
USHIRIKIANO WA MAJI
KIMATAIFA ambapo amewataka wananchi
kujitokeza katika maadhimisho hayo ambayo yanalenga katika kudumisha
ushirikiano, upandaji miti katika vituo vya maji pamoja na kutatua matatizo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment