Thursday, October 24, 2013

WANAFUNZI WAWILI WA KIDATO CHA NNE KUBAINIKA NA UJAUZITO







Na.Mwandishi wetu
 Bodi ya Shule ya sekondari ya Ibaga wilayani Mkalama imewafukuza shule wanafunzi wawili wa kike,kati ya wanafunzi 77 wa kidato cha nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wa taifa mwezi ujao baada ya kubainika kuwa na ujauzito.

Mkuu wa shule ya sekondari Ibaga,Bw Wilsoni Mchemba amesema hayo kwenye taarifa aliyotoa kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya nne ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo

Amesema shule kutokuwa na mabweni, wanafunzi  kutembea zaidi ya kilomita tano ni moja ya sababu zinazosababisha  matatizo hayo ikiwa ni pamoja na  kupata ujauzito

Aidha Bw Mchemba amewataka wazazi kushirikiana na uo

UZEMBE KWA BAADHI YA VIONGOZI HUCHANGIA KUZOROTESHA MAENDELEO



Na.Neema julius
 Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi Fatuma Hasan Toufiq amesema chanzo cha kuzorota kwa maendeleo vijijini ni kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya viongozi na kusababisha ushirikiano duni kati ya wananchi na viongozi hao

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa tarafa ya kilimatinde wilayani manyoni Bi Fatuma amesema kuwa ushirikiano duni kati ya viongizi maeneo ya vijijini ni kutokana na ushirikishwaji duni wa shuguli zenye tija kwa jamii na kusababisha miradi ya maendeleo kutofika kwa wakati katika vijiji vya wilaya ya manyoni

Aidha Bi Toufiq ameitaka idara ya ujenzi wilayani hapo kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa wilayani kabla ya mingine kuanza kutekelezwa kutokana na baadhi ya majengo kutokuwa na viwango jambo ambalo linasababishwa na  idara hiyo kwa kuendeleza uzembe na kusahau kutembelea maeneo ya vijijini

Kwa upande mwingine amewataka viongozi wa idara hiyo kujirekebisha ili majengo yaweze kukidhi viwango kulingana na maelekezo ya serikali

WAKAZI WA MKOA WA SINGIDA KUDUMISHA USAFI




Na.Anna chiganga
Kamati za mazingira kwenye serikali za mitaa mkoani singida zimetakiwa kuhamasisha wakazi wa mkoa wa singida kudumisha usafi katika maeneo yao kwa lengo la kuboresha manisapaa ya Singida

Akizungumza katika uzinduzi wa kamati za afya na mazingira mkurugenzi wa manspaa ya singida Bw Joseph Mchina amewataka watendaji wa mitaa na kata kuhakikisha manisipaa inakuwa katika mazingira safi na salama.

Amesema kila mtendaji wa kata atapewa lori la kubeba uchafu ili na atakayebainika kutupa taka ovyo awajibike ikiwa ni pamoja na kulipa faini

Aidha amewataka wananchi kuhakikisha wanatupa taka taka katika eneo husika pindi wanapomaliza kutumia mifuko ya Rambo ikiwa ni pamoja na kuichoma

Wednesday, October 23, 2013

MKOA WA SINGIDA WADHIBITI VITENDO VYA UHALIFU






                    MRAKIBU WA POLISI BW.JAMES KASUSURA

Na.Edson Raymond
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa minne nchini iliyofanikiwa kupambana na vitendo vya uhalifu kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha hivi karibuni.

Mrakibu  wa Polisi kutoka makao makuu Dar es salaam kitengo cha maadili James Kasusura amesema hayo wakati akizungumza na washiriki wa kikao cha siku maalum ya polisi kilichofanyika katika ukumbi wa Aquar manispaa ya Singida.

Kasusura ameyataja makosa yaliyopungua kuwa ni makosa dhidi ya ubinadamu ambayo yamepungua kwa asilimia 35, makosa dhidi ya mali yamepungua kwa asilimia 18, makosa dhidi ya maadili yamepungua kwa sailimia 13, na makosa dhidi ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 12.

Amesema kupungua kwa makosa hayo kumetokana na ushirikiano baina ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Singida, hivyo kutoa wito wa kuendelezwa kwa ushirikiano huo na hatimae kukomesha vitendo hivyo kabisa.