Friday, March 22, 2013

KAMATI YA BUNGE -TAMISEMI YAPATA HOFU SINGIDA


SINGIDA

Kamati ya bunge tawala za mikoa na serikali za mitaa imeitaka serikali kupitia ofisi ya mkaguzi wa hesabu za serikali kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha zilizotumika kujenga kibanda cha kuchomea taka katika hospitali mpya ya rufaa mkoani Singida.

 

Akitoa maazimio ya kamati hiyo mara baada ya kupokea taarifa fupi kuhusu ujenzi wa hospitali mpya ya rufaa ya mkoa wa singiga leo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Dk Hamisi Kigwangara amesema kibanda hicho, kinaonyesha kugharimu milioni 98 na nne jambo ambalo sio sahihi ikilinganishwa na gharama halisi mara baada ya kuona mradi huo.

 

Amesema mkataba wa ujenzi unaonyesha kuwa bati zilizotumika katika ujenzi zinagharimu milioni kumi huku kukiwa hakuna uhalisia kati ya idadi ya bati na fedha iliyotumika jambo linaloonyesha mapungufu

 

Aidha amesema serikali inatakiwa kutuma fedha za kukamilisha mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ambazo zilipitishwa katika bunge takribani bilioni mbili ili kuharakisha ujezi wa hospitali hiyo

 

Kamati hiyo ya bunge imefanya ziara ya siku mbili mkoani Singida ambapo imekagua miradi pamoja na kuzungumza na sekretarieti ya mkoa na imerejea leo mjini Dodoma


Source: SR/Hawa

Ed: BM

Date;21/3/2013

 

SINGIDA

Jumla ya wahamiaji haramu 30 wameripotiwa kuingia mkoani Singida kwa kipindi cha January  2012 hadi march 2013 kinyume cha sheria.

 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari afisa uhamiaji mkoa wa Singida

Bw.Adam Mnyeke amesema wahamiaji hao wanatoka katika nchi za Ethiopia,Somalia, Burundi na Kenya na kwamba hupita njia zisizo rasmi.

 

Amesema miongoni mwa wahamiaji hao waethiopia ni 24,wasomali 3, wakenya 2 na mrundi mmoja.

 

Aidha amesema uchunguzi umebaini chanzo cha wahamiaji hao haramu kutoka katika nchi zao kuwenda nchi jirani ni  kutokana na hali ngumu ya maisha, na hali mbaya ya kiusalama katika nchi zao,na hufanya hivyo kunusuru maisha yao

 


Source: SR/Bandola

Ed: BM

Date;21/3/2013

 

SINGIDA

Wito umetolewa kwa wananchi kwa kushirikiana na vikundi vya polisi jamii katika suala la kufanya usafi katika kata ya utemini ndani ya manispaa ya Singida

 

Mtendaji wa kata  hiyo Bw. Noel Hago ametoa wito huo wakati akiongea na Standard Redio leo ofisini kwake.

 

Bw. Hago amesema hayo kufuatia siku iliyopangwa na viongozi kwa kushirikiana na  polisi kata, kufanya usafi siku ya tarehe 22 mwezi 3 mwaka huu.

 

Aidha Bw. Hago amesema wananchi wanapaswa kuonyesha ushirikiano wao dhidi ya viongozi ili kuweza kufanikisha zoezi hilo.

 

 

 


Source: SR/Hawa

Ed: BM

Date;21/3/2013

 

SINGIDA

 Chama cha wafanyabiashara, viwanda,na kilimo mkoani singida  TCCIA  kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa fedha na kukosa wafadhili.

 

Hayo yamesemwa na afisa mtendaji wa chama hicho mkoani singida Bw. Calvert Nkurlu wakati akizungumza na standard radio ofisini kwake.

 

Amesema chama hicho kilianzishwa kwa lengo la kuunganisha nguvu ya wafanyabiashara, viwanda, pamoja na wakulima wawe na sauti moja katika masuala yanayowahusu ili kuendesha biashara kwa ufanisi

 

Aidha chama mkoani Singida kina wanachama mia sita themanini na sita, idadi ambayo ni ndogo ikilinganishwa na wafanyabiashara na wakulima waliopo katika mkoa wa singida

 

Ametoa wito kwa wafanya biashara kutumia mitandao mbalimbali ili kupata habari zinazohusu biashara, kusajili majina ya biashara, pamoja serikali kukaa pamoja na wafanyabiasha ili kujadili hali halisi ya biashara
Source: Tanzania Daima

Ed: BM

Date;21/3/2013

 

BUKOBA

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wamedai kuwa Meya wao, Anatory Amani, amekuwa akiendesha shughuli zake kibabe, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha matumizi ya fedha bila kuwashirikisha.

Madiwani hao wametoa madai hayo jana mbele ya tume iliyoundwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuchunguza tuhuma za ufisadi wa miradi mitatu zinazomkabili meya huyo, ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.

Wajumbe wengine mbali na Kandoro ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi na Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Madiwani hao kwa nyakati tofauti wameiambia tume kuwa Amani amekuwa mbabe na kufikia hatua ya kuhamisha fedha kutoka mfuko wa mradi wa viwanja sh milioni 200 kwenda kulipia deni la mradi wa soko bila idhini yao.
Source: SR/E. Lyatuu

Ed: BM

Date;21/3/2013

SINGIDA

Wananchi wa kijiji cha Mandewa Kata ya Mandewa manispaa ya Singida, wametakiwa kuwa na subira kuhusu suala la kuhamishwa kwa soko la gineri

 

Mtendaji wa Kata hiyo Bw. Bakari Ntandu amesema hayo wakati akizungumza na standard radio ofisini kwake, kuhusu mikakati iliyopo ya kuhamishwa kwa soko hilo.

 

Amesema eneo linalotumika kama soko, linatumika kwa muda na wala halikupangwa maalum kwa ajili ya soko na kwamba lipo eneo husika kwa ajili hiyo na utaratibu wa kuhamia katika eneo hilo unafanyika.

 

Amesema utaratibu unaofanyika ni kusubiri kampuni ya Spencon kukamilisha mradi wa maji, kwa kuwa eneo lililotengwa kwa ajili ya soko lipo karibu na mradi wa maji unaojengwa.

 
Aidha amewataka wananchi kuwa tayari kuhama katika eneo linatumika kama soko, kwa kuwa si eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya biashara, kwa kufuata taratibu na kutoeneza uvumi kuhusu kuhamishwa kwa soko

SINGIDA YALIA NA UHABA WA CHAKULA



Na. Boniface Mpagape.

Mkoa wa Singida umeazimia kuweka kipaumbele kwa mazao yanayostahimili ukame ambayo ni mtama, uwele na viazi vitamu ili kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula.

Maazimio hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa VETA mkoni humo. Mwenyekiti wa kikao hicho, mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Ole Kone amesisitiza wakulima kulima mazao yanayostahimili ukame, ili kwenda sambamba na hali ya hewa mkoani Singida, kutokana na ukame unaoukabili mkoa huo.

 

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Dk. Kone amesema kwa zaidi ya miaka mitatu mkoa umekuwa na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 442,180 mwaka 2009/2010 hadi tani 575,228 mwaka 2012, sawa na ongezeko la asilimia 30.

 

Amesema uzalishaji wa mazao ya biashara umeongezeka kutoka tani 164,673 mwaka 2009/2010 hadi tani 289,305 mwaka 2011/12 sawa na ongezeko la asilimia 76, na kwamba mafanikio hayo yanatokana na Mkoa kuteua na kufanya juhudi ya kuendeleza mazao ya kipaumbele kwa kuzingatia hali ya hewa. Ameyataja mazao yaliyochaguliwa kwa ajili ya chakula ni mtama, uwele, viazi vitamu na mikunde na mazao ya biashara ni alizeti, pamba, vitunguu na asali.

 

Wajumbe wa kikao hicho kwa kauli moja, wameazimia kuweka msisitizo wa kuzalisha mazao hayo na kwamba uhamasishaji ufanyike ili wakulima washiriki kikamilifu katika kuzalisha mazao hayo.

Aidha, wajumbe wa kikao hicho wamependekeza sheria ndogo ndogo  zitungwe katika kila halmashauri mkoani Singida, ili kuhakikisha kila kaya inakuwa na hekari walau tatu za mazao yanayostahimili ukame, ambayo ndiyo mkobozi kwa wakulima kuondokana na tatizo la uhaba wa chakula. Suala la matumizi mabaya ya chakula pia limejadiliwa katika kikao hicho na wakulima wametakiwa kutumia vizuri chakula wanachokipata.

 

Wajumbe wa kikao hicho pia wamejadili taarifa ya maendeleo ya elimu mkoani Singida, ambapo imeelezwa kuwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 mkoa wa Singida ni mabaya. Afisa elimu wa mkoa wa Singida Bi. Fatuma Kilimia amesema mkoa umeweza kufaulisha daraja la kwanza hadi la nne wanafunzi 2272, sawa na asilimia 23.8 kati ya wanafunzi 9,536 waliofanya mitihani hiyo.

 

Kutokana na takwimu hizo, amesema wanafunzi 7264 sawa na asilimia 76.2 walifeli kwa kupata daraja sifuri.

Thursday, March 21, 2013

MESSAGE ON THE INTERNATIONAL DAY OF FORESTS


 
the UN SECRETARY-GENERAL

--

MESSAGE ON THE INTERNATIONAL DAY OF FORESTS

21 March 2013

 

Forests are vital for our well-being.  They cover nearly a third of the globe and provide an invaluable variety of social, economic and environmental benefits.  Three-fourths of freshwater comes from forested catchment areas.  Forests stabilize slopes and prevent landslides; they protect coastal communities against tsunami and storm.  More than 3 billion people use wood for fuel; some 2 billion people depend on forests for sustenance and income, and 750 million live within them. 

 

By proclaiming the International Day of Forests, the United Nations has created a new platform to raise awareness about the importance of all types of forest ecosystems to sustainable development. 

 

Forests are often at the frontlines of competing demands.  Urbanization and the consumption needs of growing populations are linked to deforestation for large-scale agriculture and the extraction of valuable timber, oil and minerals.  Often the roads that provide infrastructure for these enterprises ease access for other forest users who can further exacerbate the rate of forest and biodiversity loss. 

 

Forests are also central to combating climate change.  They store more carbon than is in the atmosphere.  Deforestation and land-use changes account for 17 per cent of human-generated carbon dioxide emissions.  As weather patterns alter due to climate change, many forested areas are increasingly vulnerable.  This underlines the urgency of a global, inclusive, legally binding climate change agreement that will address greenhouse gas emissions and encourage the protection and sustainable management of forests.

 

Notwithstanding these immense challenges, there are encouraging signs.  The global rate of deforestation has decreased by almost 20 per cent in the past decade.  We need now to intensify efforts to protect forests, including by incorporating them into the post-2015 development agenda and the sustainable development goals. 

 

On this first International Day of Forests, I urge governments, businesses and all sectors of society to commit to reducing deforestation, preventing forest degradation, reducing poverty and promoting sustainable livelihoods for all forest-dependent peoples. 

 

Tuesday, March 19, 2013

TTCL YAAHIDI KUSHIRIKIANA STANDARD RADIO FM


VIONGOZI WA MAKAMPUNI YA STANDARD VOICE LIMITED NA TTCL MKOANI SINGIDA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KIKAO CHA KILICHOKUWA KIKIJADILI NAMNA TTCL INAVYOWEZA KUTUMIA RADIO KAMA NJIA MPYA YA MAWASILIANO BAINA YAKE NA WATEJA KATIKA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA WA KAMPUNI HIYO KUBWA YA MAWASILIANAO YA SIMU TANZANIA



Wawili katikati ni Bw. James Japhet Daud (kushoto) mkurugenzi wa Standard Voice LTD na kulia aliyevaa koti Ni Bw. Mwambene Meneja wa TTCL mkoa wa Singida. picha na. Prosper Kwigize (meneja wa Standard Radio fm) 90.10 MHz SINGIDA